Orodha ya miji ya Pwani inayokua kwa kasi lakini Serikali imeshindwa kwenda nayo sambamba

Orodha ya miji ya Pwani inayokua kwa kasi lakini Serikali imeshindwa kwenda nayo sambamba

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Orodha hii hapa.
Kongowe, hapa ni mpakani mwa Dar na Pwani, kuna movement kubwa sana ya watu, magari mengi na junction ya kutoka Kigamboni kwenda Mkuranga au Mbagala.

Mwandege hapa iliwekwa kituo cha mabasi ya mikoa ya Kusini,kiwanda kikubwa cha Bakhresa kipo hapa. Kuna biashara nyingine sana hapa.

Vikindu hapa kuna ongezeko kubwa sana la wahamiaji viwanja ni vidogo bei rahisi kiasi kila mtu ana mudu gharama. Kuna viwanda na makaazi mengi sana. Katika barabara ya Kilwa ukiacha Mbagala basi Vikindu inafuata kwa biashara.

Kisemvule. Kuna kiwanda na mabati, viwanda vya saruji,kiwanda cha kuunganisha pikipiki n.k makaazi ni mengi sana. Gari za eicher na tata toka gerezani kkoo zinapiga ruti moja kwa moja mpaka Kisemvule ni eneo linalokuwa kwa kasi sana.

Pamoja na hayo bado serikali haijaona umuhimu wa kupanua njia na kuwa hata nje 4 tu badala ya 8 kaka Kimara Mbezi.

250208122351460.JPG
250208122328763.JPG

ikitokea gari kukwama njiani basi siku imeishia hapa.

miaka 10 iijayo hali itakuwaje?
 
kuna upande mwingine wa bagamoyo nayo inakuwa sana
 
Upande wa njia ya kwenda Lindi na Mtwara kunakua kwa kasi. Na uchumi wa gas utakufanya kukue zaidi.

Serikali ipo hata huko. Ila itakuja rasmi baada ya nyinyi kuthibitisha pasipo shaka yoyote kwamba miji yenu inakua 😂😂😂😂😍
 
Back
Top Bottom