Pengine kweli ni 'subjective' na sio fair kama inavyosemwa na wasomi wengi hasa wa nchi zilizo katika nafasi za chini. Lakini, ngoja niorodheshe vigezo vilivyotumika kupata orodha hii na tuone kipi si sahihi kutumika katika kupanga, HASA VYUO VYETU. Nitaviweka kwa lugha waliypitumia wao na asilimia zake kwenye mabano.
1. Teaching: The learning environment (30%)
2. Research: Volume, Income and Reputation (30%)
3. Citations: Research influence (30%)
4. Industry Income: Innovation (2.5%)
5. International Outlook: Staff, Students and Research (7.5%)
Ni kigezo kipi ambacho wanazuoni wa Kitanzania wasemacho sio sahihi kuvi-rank vyuo vyetu? Tuache kujitetea na tuliangalie hili katika ukweli wake na kulitafutia ufumbuzi.