Orodha ya wachezaji wa Simba na mishahara yao, Niyonzima anaongoza

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299


Mashabiki wengi wa soka hupenda kujua mishahara ya wachezaja mbalimbali, lakini kwa upande wa Tanzania, mishahara hii huwa ni siri sana. Si mishahara tu, hata ada za uhamisho kwa wachezaji hawa huwa haziwekwi hadharani kama inavyokuwa kwa wanaocheza soka barani Ulaya.


Taarifa ambazo hazijathibitisha na klabu ya Simba zimesambaa mitandaoni zikionyesha majina ya wachezaji wa Simba pamoja na mishahara wanayolipwa.


Katika orodha hiyo, Haruna Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu akitokea Yanga analipwa Tsh milioni 8.7 huku Emmanuel Okwi naye aliyerejea klabuni hapo akishikilia nafasi ya pili kwa mshahara wa Tsh 7.6 na John Bocco liyetokea Azam akilipwa Tsh 6.9 milioni.




Chanzo: Swahili Times
 
Asee, kuendesha hizi klabu ni gharama kweli kweli.
 
Hii taarifa ni ya kale sana, Meddie Kagere umemwona hapo?


Sasa hivi watu tunalipa Mil 19 ila iwe siri yenu.
 
Maisha haya jamani,kumbe kuna kipindi Mavugo alikuwa anamzunguka mara mbili kwny mshahara Kichuya,Eti leo wanamwita kibonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…