Orodha ya Watanzania waliosimama kupinga uwekezaji wa DP World; tuwataje historia iwahukumu au kuwapa maua yao

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nawiwa kuweka hapa kumbukumbu za wote waliotetea na kupinga kwa nguvu zote uuzwaji wa bandari. Majina yao yakiwa hapa yatasaidia waandishi wa vitabu na makala kwa siku zijazo kupata refference na kuona kama maono yao ya kupinga yalikuwa sahihi au hayakuwa sahihi. Naomba nianze kuwataja wachache.
1. Natambua nguvu aliyotumia kijana Martini Maranja kusambaza uvumi wa mkataba ambao baadaye ilikuja kubainika mkataba ni uliovuja ulikuwa mkataba halisi.
2. Shangaz Maria Sarungi amefanya kazi kubwa kuhabarisha na kufungua majadiliano ambayo yameweza kusaidia kutoa elimu kwa umma lakini pia kuwafungua macho walio wengi. Mijadala yake imerekodiwa hivyo sauti na maandishi vitakuwa vimehifadhiwa vyema kwa matumizi ya baadaye
3. Freeman Mbowe alitoa hotuba kali na yenye kuchambua hoja mbalimbali ikiwemo kuweka msingi wa kilichozua mjadala mkubwa cha bandari za Zanzibar vs bandari za Tanganyika. Hotuba hiyo ilizaa mjadala mkali ambao bado hakuna aliyeweza kuuzima.
4. Dr. Wilbroad pamoja na kuwa balozi lakini alipoona hali si shwari aliweka utaifa mbele; akaweka diplomasia pembeni na kusimama kwenye nguvu ya imani yake hadi kukamatwa na uhaini. Aidha hata baada ya kuwekwa mahabusu bado msimamo wake haukubadilika.
5. Wakili Mwabukusi aliyeshirikiana na wasomi baadhi kwenda kuupinga mradi huu mahakama nao wanastahili kuandikwa kwa njia nyingine.
6. Majaji wakiongozwa na Jaji Ndunguru historia itawakumbuka kwa kupinga vipengele vya mkataba kwa maandishi; hukumu yao inasaidia taifa kuandika kwa manufaa ya kizazi cha kesho kuhusu aina ya watawala na wasomi waliokuwemo karne ya 21.
7. Mhe. Jaji Warioba na Butiku wanawasilisha wazee wachache ambao walitoka adharani na kusema kwa hili hapana.
8. Karibu wa TEC ( Mzee wetu Kitima) ametimiza wajibu wake; ameweka kumbukumbu zote muhimu kwa niaba ya TEC pamoja na kutupa majina ya waliosimama kiroho kupinga mkataba huu.
9. Tundu Lisu sina haja hakumweleza sana kwa sababu hata nisipoeleza anajieleza kwa historia yake juu ya rasilimali za Taifa.
10. Godbless Lema kwenye hili yupo ila hayupo kwenye vibe kiviile..........

Tuendelee tuwaleta wanaoitwa majasiri leo kwa kumbukumbu za kesho: yawezekana wanaona vyema au wamepotoka hivyo tujipe muda wakuwatambua ili kesho tuwakumbushe au tuwakumbuke
 
Mitandao ya Kijamii: Clubhouse(s), JamiiForums, Twitter, Facebook na Online YouTube channels yenyewe ijengewe minara; ikiwezekana kwenye round abouts za kila mkoa; zimefanya kazi nzuri sana ambayo main stream media zimeshindwa
 
Nawiwa kuweka hapa kumbukumbu za wote waliotetea na kupinga kwa nguvu zote uuzwaji wa bandari. Majina yao yakiwa hapa yatasaidia waandishi wa vitabu na makala kwa siku zijazo kupata refference na kuona kama maono yao ya kupinga yalikuwa sahihi au hayakuwa sahihi. Naomba nianze kuwataja wachache.
1. Natambua nguvu aliyotumia kijana Martini Maranja kusambaza uvumi wa mkataba ambao baadaye ilikuja kubainika mkataba ni uliovuja ulikuwa mkataba halisi.
2. Shangaz Maria Sarungi amefanya kazi kubwa kuhabarisha na kufungua majadiliano ambayo yameweza kusaidia kutoa elimu kwa umma lakini pia kuwafungua macho walio wengi. Mijadala yake imerekodiwa hivyo sauti na maandishi vitakuwa vimehifadhiwa vyema kwa matumizi ya baadaye
3. Freeman Mbowe alitoa hotuba kali na yenye kuchambua hoja mbalimbali ikiwemo kuweka msingi wa kilichozua mjadala mkubwa cha bandari za Zanzibar vs bandari za Tanganyika. Hotuba hiyo ilizaa mjadala mkali ambao bado hakuna aliyeweza kuuzima.
4. Dr. Wilbroad pamoja na kuwa balozi lakini alipoona hali si shwari aliweka utaifa mbele; akaweka diplomasia pembeni na kusimama kwenye nguvu ya imani yake hadi kukamatwa na uhaini. Aidha hata baada ya kuwekwa mahabusu bado msimamo wake haukubadilika.
5. Wakili Mwabukusi aliyeshirikiana na wasomi baadhi kwenda kuupinga mradi huu mahakama nao wanastahili kuandikwa kwa njia nyingine.
6. Majaji wakiongozwa na Jaji Ndunguru historia itawakumbuka kwa kupinga vipengele vya mkataba kwa maandishi; hukumu yao inasaidia taifa kuandika kwa manufaa ya kizazi cha kesho kuhusu aina ya watawala na wasomi waliokuwemo karne ya 21.
7. Mhe. Jaji Warioba na Butiku wanawasilisha wazee wachache ambao walitoka adharani na kusema kwa hili hapana.
8. Karibu wa TEC ( Mzee wetu Kitima) ametimiza wajibu wake; ameweka kumbukumbu zote muhimu kwa niaba ya TEC pamoja na kutupa majina ya waliosimama kiroho kupinga mkataba huu.
9. Tundu Lisu sina haja hakumweleza sana kwa sababu hata nisipoeleza anajieleza kwa historia yake juu ya rasilimali za Taifa.
10. Godbless Lema kwenye hili yupo ila hayupo kwenye vibe kiviile..........

Tuendelee tuwaleta wanaoitwa majasiri leo kwa kumbukumbu za kesho: yawezekana wanaona vyema au wamepotoka hivyo tujipe muda wakuwatambua ili kesho tuwakumbushe au tuwakumbuke
13.The burning spear.
14.Maaskofu wote wa TEC.
15.Askofu Mwamakula.
16. Diaspora
 
Humu ndani tusimsahau dada yetu mpendwa Faiza Foxy, naye amejitahidi sana kuelezea umahiri wa dp world katika mkataba wa bandari
 
Hiyo ni zero IQ aka ili mradi Leo tumeshiba kesho itajihangaikia.
Wanangalia ugali wa leo bila shaka watakuja na maneno mengi, mipasho, ngonjera zisizo na kichwa wala miguu.

Mara moja moja wanaongea kizalendo zaidi moja kati ya kila mabandiko yao mia moja.
 
13.The burning spear.
14.Maaskofu wote wa TEC.
15.Askofu Mwamakula.
16. Diaspora
Haha, hadi The burning spear. mkuki wako unaunguza na kuchoma wakati huohuo. Pokea maua yako kwa niaba ya JF, Tanzania.

Mbatia, NCCR mageuzi wapo kwenye kundi la wazalendo.
 
Back
Top Bottom