Oscar Academy: Baada ya Smith kumpiga Rock, aliombwa aondoke akagoma, tutachukua hatua za kinidhamu dhidi yake

Oscar Academy: Baada ya Smith kumpiga Rock, aliombwa aondoke akagoma, tutachukua hatua za kinidhamu dhidi yake

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Waandaaji wa tuzo za Oscar wanasema baada ya smith kufanya fujo na kumpiga Rock, aliombwa aondoke lakini akagoma.

Oscar Academy wanasema watamchukulia smith hatua za kinidhamu kwa kufanya fujona pia kudhalilisha hadhi ya tuzo hizo za kimataifa.

Watu wengi wanasema alichokifanya Smith kimezidi kuharibu picha ya watu weusi na kutengeneza mazingira ya kuwapa sababu watu kuendelea kusema kwamba watu weusi ni watu wa fujo, wasio wastaarabu na wanaopenda ghasia, na ugovi.

Mcheza kikapu mkongwe bwana Kareen Abdul Jabbar amesema alichokifanya Smith kimeharibu na kubomoa hadhi ya watu weusi Duniani kote kwa kutuonyesha watu weusi kua ni watu wasio wastaarabu, wagomvi.

Mapenzi yamemharibu Will.

Kwamba kasababisha weusi tuonekane watu wa fujo?

Well weusi wameuawa na weupe for years kuanzia Emmet Till, Rodney King mpaka George Floyd na hamna mtu mweupe aliwaambia weupe wenzake kwamba "Mauaji uliyofanya yamesababisha watu weupe tuonekane wauaji"
 
Ila tukio la Jada kutaniwa maradhi yanayomsibu, wanawake na Dunia imekaa kimya ? Lakini mtu kuwa judged kwa tukio la muda huo kama kilichotokea kwa Will lakini siyo kumaanisha Will ni mtu mbaya sana.

Bado tunaona ubaguzi upo na Waafrika bado fikra zetu inaonyesha kabsa roho za utumwa zinatutawala.

Sikubaliani na tukio la Will isipokuwa mtu yoyote angeweza ku_react na ndiyo maana tunaambiwa tuwe na "kiasi".

Hiyo haimuondoi Will Smith kuwa ni msanii nguli. Ni vema wachekeshaji wakabuni mtindo mpya wa kuwasilisha ujumbe wa kwa mtindo tofauti.
 
Eti inaharibu taswira ya Mtu mweusi....
Yaani mtu akutanie uumie ushindwe kureact kwa kua ni Mtu mweusi Wazungu watakuona ni Mkorofi,

Utumwa umeathiri sana, sijui lini Mtu Mweusi ataweza kujikomboa juu ya Utumwa wa Fikra.
 
Kweny hili niko na will smith

Kutania mtu kwa maradhi yake sio fair tena mkewe wake mbele ya kadamnasi na watu wakacheka sana just imagine jada alifeel vipi.

Si mnasemaga wanaume wapo kwa ajili ya kutoa protection kwa wanawake na kufeel secure.

It was responsibility will kustand na mkewe kwa hali yeyote.

Hili swala hao academy waliache lipite kama lilivyo kwa heshima ya will,jada na huyo chris rock.

Hii ishu hata angekua denzel Washington au samuel L jackson angechapa ngumi tu Chris Rock.

Matani ya kijinga tuyaache
 
Ila tukio la Jada kutaniwa maradhi yanayomsibu, wanawake na Dunia imekaa kimya ? Lakini mtu kuwa judged kwa tukio la muda huo kama kilichotokea kwa Will lakini siyo kumaanisha Will ni mtu mbaya sana. Bado tunaona ubaguzi upo na Waafrika bado fikra zetu inaonyesha kabsa roho za utumwa zinatutawala.

Sikubaliani na tukio la Will isipokuwa mtu yoyote angeweza ku_react na ndiyo maana tunaambiwa tuwe na "kiasi". Hiyo haimuondoi Will Smith kuwa ni msanii nguli. Ni vema wachekeshaji wakabuni mtindo mpya wa kuwasilisha ujumbe wa kwa mtindo tofauti.
Chris hakumtania kwa maana ya maradhi. Alimtania kwa maana ya kunyoa. Jada amenyoa nywele zake na ile inamfanya kuwa na muonekano mzuri wa kucheza character ya G.I.Jane.

Huyu character huwa ananyoa sababu anakuwa kwenye mishe za kijeshi. Sasa Chris alipomuona Jada kanyoa nywele akasema kwa muonekano huo anategemea kumuona anaplay character ya G.I.Jane sababu atapendezea.....

Sasa hapo mtu amefanya mzaa na ugonjwa wa mtu.....?! View attachment 2170176
images%20(64).jpg
 
Watupumzishe...Smith..Smith..😏
 
Ila tukio la Jada kutaniwa maradhi yanayomsibu, wanawake na Dunia imekaa kimya ? Lakini mtu kuwa judged kwa tukio la muda huo kama kilichotokea kwa Will lakini siyo kumaanisha Will ni mtu mbaya sana. Bado tunaona ubaguzi upo na Waafrika bado fikra zetu inaonyesha kabsa roho za utumwa zinatutawala.

Sikubaliani na tukio la Will isipokuwa mtu yoyote angeweza ku_react na ndiyo maana tunaambiwa tuwe na "kiasi". Hiyo haimuondoi Will Smith kuwa ni msanii nguli. Ni vema wachekeshaji wakabuni mtindo mpya wa kuwasilisha ujumbe wa kwa mtindo tofauti.
Naona wanamuonea Will..Rock ndio alianza uchokozi hata ningekua mimi ama mtu mwingine lazima angekasirika.
 
Kwanini will smith ahukumiwe au ajadiliwe kwa rangi yake ya ngozi? kwanini ajadiliwe kwa uafrika wake? kwanini asihukumiwe yeye kama yeye? hilo tukio lingefanywa na mzungu lingemjadili huyu mzungu kwa uzungu wake au kwa rangi yake ya ngozi?
Kuna mijitu mibaguzi sana.
 
Ila tukio la Jada kutaniwa maradhi yanayomsibu, wanawake na Dunia imekaa kimya ? Lakini mtu kuwa judged kwa tukio la muda huo kama kilichotokea kwa Will lakini siyo kumaanisha Will ni mtu mbaya sana. Bado tunaona ubaguzi upo na Waafrika bado fikra zetu inaonyesha kabsa roho za utumwa zinatutawala.

Sikubaliani na tukio la Will isipokuwa mtu yoyote angeweza ku_react na ndiyo maana tunaambiwa tuwe na "kiasi". Hiyo haimuondoi Will Smith kuwa ni msanii nguli. Ni vema wachekeshaji wakabuni mtindo mpya wa kuwasilisha ujumbe wa kwa mtindo tofauti.
Chris rock Mimi simkubaligi mda sababu he is too personal ndo staili yake ya uchekehaji amewafanyia wengi Ila will Smith akaamua kuovereacting

Jamaa abadilike anachofanya ni bullying na sio comedy
 
Back
Top Bottom