Oscar Baumann mchoraji ramani wa zamani

Polycarp Mdemu

Senior Member
Joined
Jun 2, 2019
Posts
165
Reaction score
209
- Moja Ya Watu Muhimu katika Historia Ya Tanganyika na Zanzibar.

- Jamaa alikua ni Mzaliwa wa Taifa La Austria, Na Alikua Mjuzi katika Taaluma mbili tofauti Kwanza Alisoma Cartography elimu ambayo Mtu hubobea Katika Kusoma Ramani na Kutafsiri Ramani ama Kusoma Ramani, Mtu ambaye anakua amesomea Mambo haya huitwa "cartographer" pia Jamaa Alisoma mambo ya Ethnography Hili ni somo la Tafiti za Tamaduni tofauti, Ama utofauti wa Mienendo ya Watu Binafsi wa Eneo fulani na Jingine, Hapa mtu hutafiti mpaka Matukio ya Kitamaduni ili Kulinganisha ama Kutofautisha, Mtu anayesomea mambo haya huitwa "ethnographer"

- Kwa Maana Hiyo Bwana Oscar Yeye Alikua ni ethnographer pia akawa ni cartographer, Ni sawa na Mtu Kuwa Muhandisi wa Majengo, Hapohapo Ukawa Msanifu wa Majengo, Field Mbili tofauti lakini zinafanya kazi zinazofanana.

- Huyu Jamaa Alisoma Mambo hayo Katika chuo Kikuu Cha Viena, Chuo cha Zamani zaidi katika Nchi zinazoongea Kijerumani (German-speaking world) ambacho kilianzishwa mwaka 1365 na Duke Rudolph IV na Mpaka sasa Ni moja ya Vyuo Vikubwa Ulaya.

- Alipomaliza Masomo yake Matokeo yake yalikua mazuri hivyo alipata nafasi ya kuwa Katika Kundi la Austrian exploratory ambalo liliongozwa na Oskar Lenz mwaka 1885 walipokuja Africa Kuchunguza Bonde la Mto Congo (Congo Basin) Na Akawa mtu pekee aliyefaulu Kuchora Ramani ya Mto Kongo Halisi, Lakini Aliugua sana Hivyo akarudi Kwao Austria.

- Mwaka 1886 Alirudi Tena Africa, Wakati Huu alifika katika Kisiwa cha Fernando Po ambacho kwa sasa kinaitwa Bioko, Alifika Hapa Kuchunguza Utamaduni wa Jamii ya Hiki Kisiwa na Jiografia yake, Utafiti huu ulimsaidia aliporudi kwao Kuandika Tasnifu ambayo Ilimfanya apewe Shahada ya Uzamivu (Phd) Kutoka chuo Kikuu cha Leipzig mwaka 1888

- Mwaka Huo Huo 1888 Oscar "Akayakanyaga" akapewa Mwaliko na Bwana mmoja wa kuitwa Hans Meyer kuja Tanganyika ambako Wajerumani walikua washatia timu na Kutawala.

- Huyu Ndio Alichora Ramani zilizofikia Uhalisi za Upande wa Burundi, Rwanda na Tanganyika na Zanzibar, Alichora Ramani za Maeneo yote hayo.

- Akachora Ramani ya Mlima Kilimanjaro, Milima ya Usambara, Lakini Kabla kazi haijaenda sana Alikamatwa na Msafara wa Askari wa Vita ya Abushiri "Abushiri Revolt" ambao walipinga Ukoloni, Akawa Mfungwa wa Mfanyabiashara wa Tanga Abushiri ibn Salim al-Harthi ambaye ndio Kiongozi wa Vuguvugu hilo, Lakini Oscar Alimuomba Abushiri kumuhifadhia Karatasi na nyenzo Muhimu zisiharikike, lakini kwa mujibu wa Afisa Mwingereza Edmund Fremantle alisema "Wameibiwa, kuvuliwa nguo, na kutendewa kila aibu, Pia wamepoteza vyote, Vifaa vyao na makaratasi uchunguzi, mbaya zaidi hawaonekani kuwa wabaya" Lakini Baada ya Fidia kubwa kutolewa, Abushiri Aliwaachia Watafiti wale.

- Baada ya Kutoka Kifungoni Oscar Aliandaa watu 200 ili kufanya nao kazi, Aliuita msafara huo "Maasai Expedition" alitembea na watu hao Kokote alikoenda.

- Kupitia msafara huu alifanya Mambo mengi ambayo Yanaheshimiwa Mpaka Leo, mwaka 1891 mpaka Mwaka 1893 alifanya kazi za Kuchora Ramani Tu, Akawa Ndio Mzungu wa Kwanza Kufika Rwanda, Miaka Hiyo Hiyo akawa ndio mzungu wa Kwanza Kufika Ziwa Eyasi, Ziwa Manyara na kuchora Ramani za maeneo hayo.

- Pia Akawa Mzungu wa Kwanza Kufika Bonde La Ngorongoro, Akaendelea mpaka Kutafuta chanzo cha Mto Kagera, Na hapa ndipo alipata Chanzo Cha Mto Nile ambacho ni Halisi mpaka leo, Japo Haandikwi kuliko waliokuja Baada yake,

- Moja ya Matokeo na Mafanikio ya Msafara huo, Alipomaliza aliandika kitabu alichokiita "Durch Massailand zur Nilquelle" yaani "Kutoka Ardhi ya Wamasai mpaka Chanzo cha Mto Nile" hiyo ilikua mwaka 1894.

- Mwaka 1896 serikali ya Austria- Hungaria ilimpa ubalozi wa Zanzibar, Lakini huko aliteswa sana na Magonjwa ya Kuambukizwa, Hasa Malaria, Akafa akiwa na Miaka 35 tu.

- Mipaka yetu tunapopata uhuru ilikua ni Uhalisia wa Huyu Jamaa, Lakini sidhani kama kuna mahali labda anapewa heshima ama hata kukumbukwa, Maana Hata Reli zilizojengwa Enzi za Ukoloni uchunguzi ulipatikana katika Ramani za Huyu Jamaa.

- Kwa Wenzetu wanaotambua mchango wake, Huko Vienna Kuna Barabara inaitwa Baumannstraße ni Kumbukumbu ya huyu Jamaa, Huko nchini Togo, Point ya Juu zaidi Kutoka usawa wa Bahari initwa Baumannspitze kwa sasa unajulikana kama Mlima Agou.

Polycarp Mdemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…