Oscar Kambona: Kijana aliyegeuka mwiba kwa mwalimu wake

Oscar Kambona: Kijana aliyegeuka mwiba kwa mwalimu wake

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
FB_IMG_1583131500284.jpeg
Na: Peter Mwaihola

Vijana Ni nguzo ya Taifa hivyo Taifa lolote halina budi kua na vijana wenye weledi wa Mambo pamoja na Utashi katika kufanya Mambo Jambo ambalo linaweza kuwapa historia kubwa hata baada ya mwisho wa uhai wao kitaifa na Kimataifa.

Tanzania Kama Taifa liliasisiwa na Vijana makini kwa wakati ule Oska Kambona Ni mmoja tu Kati ya vijana walio Andika historia Ya taifa Hili Kabla na Mara baada ya uhuru.

Hii ilikua Ni kutokana na harakati zake katika kudai Uhuru na hata baada ya uhuru akiendelea kuleta changamoto ya mawazo chanya ambayo Hadi Leo imekua misingi ya Taifa hili.

Kambona Alizaliwa mnamo agost 13 1928 katika kijiji kidogo cha kwambe kilichopo katika fukwe za ziwa nyasa karibu na mbamba bay wilaya ya Nyasa.

Alikua ni mtoto wa kiume wa bwana David Kambona na Bi Miriam Kambona, baba yake alikua ni miongoni mwa waafrika wa mwanzo kupewa cheo cha uchungaji katika kanisa la kianglikana Tanganyika.

Oska kambona alipata elimu yake ya msingi chini ya mti wa mwembe ambao hadi sasa ungali umesimama huko kijijini kwao alisomeshwa na wazazi wake pamoja na mjomba ambae nae alikua mwalimu.

Baada ya hapo alijiunga na shule ya kati ya mtakatifu Barnabas liuli (st Barnabas Middle school) ambayo haikua mbali sana kutoka kijijini kwao.

Oska kambona alibahatika kulipiwa ada na askofu wa kanisa la kianglikana Tanganyika kwani baba yake hakua na uwezo wa kumudu kulipa ada hiyo ambayo ilikua ni takribani paundi 30 za kiingereza kwa mwaka. Inasemekana Kambona alimshawishi askofu huyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma sara ya baba mtakatifu kwa lugha ya kiingereza.

hii ikawa hatua nyingine njema kwa kambona kwani baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora ambapo kwa mara ya kwanza alikutana na na Julius Nyerere ambae alikua tayari amefundisha shule ya mtakatifu maria ya mjini Dodoma.

Kambona alikua ni kijana mwenye ushawishi na umaarufu mkubwa baada ya mwalimu Nyerere yeye alifuata mawazo yake juu ya ukombozi yaliamfanya akubalike na kuteuliwa kua katibu mkuu wa TANU huku mwalimu Nyerere akiwa mwenyekiti.

Alishirikiana kwa ukaribu sana na watanganyika wengine kupigania uhuru mnamo mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mwingereza .

Baada ya uhuru Kambona alibaki kua na ushawishi mkubwa hata baada ya muungano ambao ulizaa Tanzania na ikaaminika kua angekua rais baada ya mwalimu nyerere kustaafu au kung’atuka madarakani kwa sababu yoyote ile.
Uwezo wake katika kuongoza ulithibitika Pale alipokua waziri wa ulinzi alipo watuliza wanajeshi ambao walifura wakitaka kuipindua serikali mwaka 1964 ambapo Rais Nyerere na makamu wake Rashidi kawawa walipelekwa mafichoni sehemu salama kutokana wanajeshi kutaka kuwadhuru.

"Asante Sana ahsant ndugu yangu" hii ndiyo ilikua kauli pekee ya Rais Nyerere Baada ya upepo huo wa jaribio la Mapinduzi kupita alijitokeza hadharani kumshukuru kambona kwa kazi kubwa aliyoifanya kuwatuliza wanajeshi.
Viongozi wawili hawa walianza kutofautiana miaka michache baada ya uhuru . mgawanyiko wa kwanza ulikua mwaka 1964 wakati wa jaribio la mapinduzi na mgawanyiko wa pili ulikua mwaka 1965 Tanzania ilipo ingia rasmi kwenye mfumo wa chama kimoja.

Kama mmoja wapo wa baraza la mawaziri Oscar alipinga mabadiliko hayo akidai kua hakukua na mikakati wala mwongozo kwa serikali kikatiba kutawaliwa na chama kimoja huku hofu yake kubwa ikiwa katiba ilikua haina ulinzi kama nchi ama serikali itageuka kuwa ya kidikteta.

Mwaka 1967 baada ya azimio la arusha lililo adhimia ujamaa na kujitegemea, kambona alikua haamini katika ujamaa hivyo alipingana na mfumo huu akiitaka serikali kuanzisha sehemu chache za matazamio kama mfumo huu ungekizi maendeleo kitaifa.

Utofauti mkubwa wa Rais Nyerere na Kambona ulikua kwenye masuala ya kisera ambapo kambona alikua si muumini wa sera ya ujamaa na kujitegemea ambayo Nyerere alikua akiamini.

Kuna msemo wa kiswahili usemao "Fahari wawili hawakai zizi moja" mnamo mwezi julai 1967 Kambona aliondoka nchini akiambatana na mke wake pamoja na watoto wake kuelekea London nchini uingereza kuondoka kwake kuliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo radio, magazeti na runinga.

“Mwacheni aende” hiyo ndio sauti kuu iliyotoka katika kinywa cha mwalimu nyerere aliposikia kuondoka kwake, pia alisisitiza kua Kambona aliondoka na kiasi kikubwa cha pesa ambacho hakikuendana na mshahara wake "je alipata wapi mapesa yote yale" Nyerere alihoji Kwani kulikua na tetesi kua alijitajirisha alipokua ofisini kupitia pesa za harakati za ukombozi wa bara la afrika chini ya umoja wa afrika (OAU) Ambapo yeye alikua mwenyekiti wa kamati hiyo ya ukombozi kusini mwa Afrika.

Nae kambona hakutaka kushindwa mara moja alijibu tuhuma hizo mbele ya umma wa wana habari huko ughaibuni akisema “sina hatia yoyote juu ya hili iwapo kuna mwenye ukweli basi anifanyie uchunguzi na anianike hadharani”.
Muda mfupi mwaka uliofuata wa 1969 kambona alitangaza kua atafanya mapinduzi mnamo mwezi wa oktoba lakini Bodo mpango wake ukakwama kwani wahisani wake wote walitiwa nguvuni na kambona Alishitakiwa kwa Uhaini licha ya kua ughaibuni na hukumu ikasomwa mahakamani.

Wakati wa hukumu mmoja wa washirika wake “John Chifupa” aliulizwa je ulimaanisha nini uliposema unataka kummaliza Nyerere Chifupa akakana akisema “la hasha hakimu mimi sikumaanisha kummaliza Nyerere kimwili bali nilimaanisha nataka kummaliza kisiasa”

Baada ya kesi hiyo kuunguruma miaka kadhaa kambona aliendelea kua mwiba kwa serikali ya mwalimu Nyerere akiwa huko ughaibuni mpaka pale Nyerere alipo ng'atuka madarakani.

Ilikua mwaka 1992 baada ya Tanzania kurejesha mfumo wa vyama vingi nae Kambona akaamua kurejea nyumbani na kujiunga na chama kimojawapo cha siasa baada ya kukaa uhamishoni kwa mda mrefu zaidi ya miaka 25.

licha ya kua mstari wa mbele katika kupigania uhuru miaka ya 1960 kambona alinyimwa nafasi ya kugombea uongozi katiaka chaguzi zote za miaka ya 90 ikidaiwa kua si mtanzania bali mmalawi, wengine walisikika wakisema ni raia wa msumbiji, Kambona alijibu mapigo kwa kumwambia Nyerere nae si mtanzania bali mnyarwanda.

Mnamo mwezi julai 1997 huko London uingereza Oska kambona aliutoka umma wa watanzania baada ya kuugua kwa muda, Kambona amebaki katika historia Ya vijana wa wakati ule akijumuishwa na Vijana wengine jasiri wa wakati huo Kama Chifu Said Fundikira na wengine wengi walio kua mstari wa mbele katika siasa na maendeleo ya Taifa.

petermwaihola809@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere hakuwahi kumsamehe Kambona hadi siku Oscar anaiga dunia. Mwandishi mkongwe Ahmed Rajab ambae alikua na usuhuba na Mwalimu Nyerere alisema hayo katika moja ya simulizi zake

Rajab alisema Mwalimu Nyerere alikua London kwa mwaliko wa taasisi moja ya kimataifa iliyokua inajihusisha na mambo ya Demokrasia na Maendeleo, na yeye Ahmed pia alikua amealikwa kwenye mkutano ule. Wakati wote wakikutana na Mwalimu walikua wanaongea na kutaniana, kitu ambacho kinanistaajabisha, kwani Nyerere hakua na watu wengi ambao waliweza kumtania. Wengi wakimsikiliza akiwa lecture, kuwaonya, kuwasimulia na hata wao kumuuliza maswali lakini pia akiwachekesha na wakati fulani wakivumilia kutaniwa naye na sio wao kumtania

Akiwa anajitayarisha kwenda kwenye hoteli ambayo mkutano ule ulikua unafanyika, Ahmed Rajab alipokea ujumbe kutoka kwa Mohamed Mlamali Adam(mwandishi mwingine nguli) kua Oscar Kambona amefariki dakika chache tu zilizopita

Alipofika hapo Hotelini Ahmed alifanya hima kumuona Mwalimu ili ampe habari za motomoto kuhusu kifo cha swahiba wake wa zamani. Ikumbukwe kua Nyerere alikua Best Man wa Kambona kwenye harusi yake

Ahmed anaeleza kua alipompa Mwalimu habari hizo wala hakushtuka!!! Akamwambia tu "Ok, lini? Baada ya kusema hivo Mwalimu akabadilisha mazungumzo na hakuongelea tena la heri wala la shari kumhusu Oscar Kambona. Hakika Mwalimu Nyerere hakuwahi kusamamehe aliyekua wakati fulani rafiki yake kipenzi hadi sasa hivi ambapo wote wawili wapo mbele za haki
 
Pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom