Oscar Sudi hakufanya KCSE 2006, anatumia cheti cha Bob Onyango

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Afisa kutoka Baraza la Kitaifa ya Mitihani Nchini (KNEC) ameambia korti moja jijini Nairobi kuwa jina la Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi haliko kwenye orodha ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne mwaka 2006.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkuu Felix Kombo katika kesi ambayo mbunge huyo anatuhumiwa kughushi cheti cha KCSE, afisa huyo wa KNEC kwa jina Nabiki Kashu alisema cheti cha Sudi ni cha kutoka kwa shule hewa Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Nation.

Shahidi huyo alisema Sudi aliwasilisha cheti cha KCSE kutoka Shule ya Sekondari ya Highway lakini rekodi zao zinaonyesha kuwa cheti hicho ni cha mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani wake katika Shule ya Sekondari ya Parklands mwaka 2006.

Tuliulizwa kujua ikiwa mwanafunzi kama huyo alisomea KCSE 2006 katika Shule ya Sekondari ya Highway jijini Nairobi," alisema kuhusu barua kutoka kwa EACC iliyoitaka KNEC kufanya uchunguzi. Katika maelezo yake, mfanyikazi huyo wa KNEC, ambaye ndiye mkuu wa rekodi katika baraza la mitihani pia alisema mnamo 2006, hakukuwa na jina la shule kama Shule ya Upili ya Highway.
 
Amefinywa pabaya, baada ya kuropokwa vibaya juu ya serikali, siasa noma! 😂 😂 😂 😂 don't throw stones if you know your house is made of glass., 😂 😂 😂 Kenyan politics..,
 
Back
Top Bottom