DOKEZO OSHA hawajatupa vyeti vya kuhitimu mafunzo tokea 2024, tukifuatilia tunazungushwa bila majibu ya msingi

DOKEZO OSHA hawajatupa vyeti vya kuhitimu mafunzo tokea 2024, tukifuatilia tunazungushwa bila majibu ya msingi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari za leo Mdau, naomba utusaidie kupaza sauti iwafikie taasisi ya OSHA.

Wanavyuo wa NIT, Ardhi na Chuo cha Maji 2024 tulilipia pesa 30,000 kwaajiri ya mafunzo semina ya Usalama mahala pa kazi (OSHA), tulipewa mafunzo tokea siku ya 20/04/2024, lakini baada ya hapo vyeti vilichelewa kutoka mpaka wengine tumehitimu masomo.

Baadae tulipewa utaratibu wa kujisajili kwenye mfumo wa OSHA online ili tutumiwe vyeti online huko tukafanya hivyo lakini wakatumiwa wachache wengi hatukutumiwa.

Tumetoa lalamiko letu sana kwa viongozi wetu walotuchangisha pesa ila wamekuwa wakitupa majibu ya mkato sana. Baadae kwenye mwezi wa 12 wakatuma attendence ya majina machache ya mahudhurio ya semina hiyo, ajabu ni kuwa wengine walihudhuria lakini majina yao hayapo.

Mpaka sasa wengine tumehitimu tuko mikoani tumepaza sauti watupe hata sababu za kuchelewa huko lakini ni kama tumepigwa changa la macho.

Mdau tunaomba utusaidie kufikisha ujumbe huu wenda watatusikiliza tutumiwe vyeti vyetu maana tulilipia 30,000 pia.

Shukrani sana Mdau...
 
Itakua viongozi wenu waliipiga hio pesa wakalipia wachache
 
Back
Top Bottom