Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kuhusu hoja ya memba, soma hapa ~ OSHA mko wapi? Ubomoaji wa jengo la zamani la DDC Kariakoo unafanyika kiholela, ni hatari kwa usalama wa Watu
Meneja-Kanda ya Pwani wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), George H. Chali amesema:
Tumeona andiko na hayo malalamiko ya Mwananchi jana usiku (Juni 5, 2024) na tukabaini wabomoaji wamekiuka SHERIA YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI NAMBA 5 ya Mwaka 2003 na Kanuni za zake, hawakufuata utaratibu unaotakiwa.
Kwanza kabla ya kufanya ubomoaji kama huo waliokuwa wakiufanya wanatakiwa kufanya tathimini ya nini kitatokea wakati wa mchakato.
Wanatakiwa kusajili mchakato wao huo OSHA lakini wahusika hawakufanya hivyo.
Hivyo, tumezuia mchakato wote wa ubomoaji hadi wahusika watakapofuata taratibu zinazotakiwa labda kama waendelee kufanya hivyo kinyemela.