Inawezekana tumeshaandaliwa vya kutosha kukiogopa kifo ili tusifanye mambo fulani au tutekeleze matakwa ya watu fulani.
Kifo ni hatima ya kila kiumbe, na hakiepukiki.
Kifo ni adhabu ("utakufa hakika")
Kifo ni adui na hakiwezi kuwa rafiki.
Kifo hakistahiri kwa binadamu mchanga, mtoto, kijana, mtu mzima anayepaswa kufanya kazi za kuzalisha na kuitawala dunia.
Kifo ni cha binazamu aliyeisha nguvu, Mzee sana, aliyekula chumvi nyingi, aliyeisha nguvu na hana anachoweza kufanya kwa kuzalisha au kutawala.
Kwa binadamu mzee sana, kifo ni baraka kwake, ni rafiki yake, na hatima stahiki kwake, kwani jumba lake yaani mwili wake umechoka na kuchakaa kiasi cha kutohitajika duniani.
Hapo kifo chahitajika sana kwa mzee huyu, kama uhai unavyohitajika sana kwa kijana huyu.
Hapo hata jamii haistaajabu tena, haisikitiki tena, hai lii tena kwa kifo cha mzee, bali inafurahia pamoja na yeye, huyo mzee.