I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Kibao cha Ouija
Kwa kipindi cha karne na karne binadamu wamekuwa na shauku kubwa ya kuongea na wapendwa wao waliokufa au aina nyingine za roho.
Hali hiyo ilipelekea kuvumbuliwa kwa kibao (OUIJA Board) kilichosadikiwa kufanikisha miunganiko kati ya hizi pande mbili za kiulimwengu yaani ulimwengu wa kimwili na kiroho.
Kulingana na shuhuda mbalimbali zinaeleza kuwa pindi kibao hiki kitumikapo kuita roho hizi, ni hakika ishara na hata sauti za roho zilizoitwa husikika.
Lakini je, ni kweli mambo haya wasemayo hutokea au ni moja ya njia ubongo wa mwanadamu hutengeza namna na kumfanya mtu anayecheza Ouija kuhisi,kuona ama kusikia vitu visivyo vya kweli katika hali ya kawaida?