Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Ujumbe wangu leo ni kwa vijana popote walipo katika nchi yetu. Vijana wa aina zote kabisa. Wa mjini na wa vijijini. Walioelimika na wasioelimika. Kama kichwa cha habari kinavyoelezea nataka nijadili hiki kitu kwa kina nitajaribu kuelezea kwanini ni muhimu na kwanini watu wetu wa value hiki kitu ambacho ni kazi ya mikono yetu (our own creation)
Sisi kama watu ambao tuko katika ardhi hii hatujawahi kuunda taifa; Taifa tulilokuwa nalo ambalo lilikuwa linaitwa Tanganyika hatukuliunda kwa dhamira yetu wenyewe. Taifa la tanganyika lilikuwa ni zao la conquest ya mkoloni ni lazima mtambue hili. Hakuna hata mmoja miongoni mwa mababu zetu alikuwa hata na dhamira ya kuunda taifa linaloitwa Tanganyika. Kwa nguvu wajerumani walivamia na kutawala kabila moja baada ya jingine na kuunda tanganyika na kufanya koloni lake. Ni mjerumani aliyetukusanya na kututawala ni yeye aliyeunda tanganyika. Kwahiyo hatupaswi kujivunia Tanganyika. it is not our own creation. Any intelligent Man will honor Mwalimu Julius Kambarage Nyerere for the creation of Tanzania. We must celebrate this.
Kwahiyo kama taifa hatupaswi kurudi nyuma hata kidogo na kamwe tusirudi katika Tanganyika na yeyote mwenye mawazo kama hayo ni adui wa usalama wa taifa letu. Hakuna kumchekea mtu kama huyo. Kurudi nyuma kwetu na kuitaka Tanganyika kutasababisha tanganyika yenyewe isibaki salama. Haitobaki moja. Roho ile ile iliyofanya tutengane ni hiyo hiyo itakayobomoa Tanganyika isiwe moja. Taifa hili halitaki watu wanaotaka kuturudisha nyuma bali watu watakao tupeleka mbele tukiwa wamoja.
Tanganyika haikuundwa kwa dhamira yetu wenyewe bali kwa dhamira ya mkoloni na hakuna hata moja ya makabila tuliyonayo ambalo lilikubali kwa hiari yake kuundwa kwa Tanganyika. Kitu gani kitakachotokea baada ya Tanganyika kujitoa kwenye muungano kuna uwezekano wa baadhi ya sehemu kudai kujitenga baada ya tanganyika kubaki peke yake au ukabila ukamea na kuota mizizi katika taifa letu. Kwahiyo mtawala atakayetawala Tanganyika lazima atapata tabu kuviweka hivi vipande pamoja. Wanaodai tanganyika ni watu wajinga au wanadhamira mbaya ya kuua utaifa wetu. Hakuna kitu kitakachobaki kinachoitwa Tanganyika baada ya kujitoa kwenye muungano. Ni marufuku kuirudia Tanganyika. Tukirudi nyuma madhara tutakayokumbana nayo tutajuta.