Our own creation

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Ujumbe wangu leo ni kwa vijana popote walipo katika nchi yetu. Vijana wa aina zote kabisa. Wa mjini na wa vijijini. Walioelimika na wasioelimika. Kama kichwa cha habari kinavyoelezea nataka nijadili hiki kitu kwa kina nitajaribu kuelezea kwanini ni muhimu na kwanini watu wetu wa value hiki kitu ambacho ni kazi ya mikono yetu (our own creation)

Sisi kama watu ambao tuko katika ardhi hii hatujawahi kuunda taifa; Taifa tulilokuwa nalo ambalo lilikuwa linaitwa Tanganyika hatukuliunda kwa dhamira yetu wenyewe. Taifa la tanganyika lilikuwa ni zao la conquest ya mkoloni ni lazima mtambue hili. Hakuna hata mmoja miongoni mwa mababu zetu alikuwa hata na dhamira ya kuunda taifa linaloitwa Tanganyika. Kwa nguvu wajerumani walivamia na kutawala kabila moja baada ya jingine na kuunda tanganyika na kufanya koloni lake. Ni mjerumani aliyetukusanya na kututawala ni yeye aliyeunda tanganyika. Kwahiyo hatupaswi kujivunia Tanganyika. it is not our own creation. Any intelligent Man will honor Mwalimu Julius Kambarage Nyerere for the creation of Tanzania. We must celebrate this.

Kwahiyo kama taifa hatupaswi kurudi nyuma hata kidogo na kamwe tusirudi katika Tanganyika na yeyote mwenye mawazo kama hayo ni adui wa usalama wa taifa letu. Hakuna kumchekea mtu kama huyo. Kurudi nyuma kwetu na kuitaka Tanganyika kutasababisha tanganyika yenyewe isibaki salama. Haitobaki moja. Roho ile ile iliyofanya tutengane ni hiyo hiyo itakayobomoa Tanganyika isiwe moja. Taifa hili halitaki watu wanaotaka kuturudisha nyuma bali watu watakao tupeleka mbele tukiwa wamoja.

Tanganyika haikuundwa kwa dhamira yetu wenyewe bali kwa dhamira ya mkoloni na hakuna hata moja ya makabila tuliyonayo ambalo lilikubali kwa hiari yake kuundwa kwa Tanganyika. Kitu gani kitakachotokea baada ya Tanganyika kujitoa kwenye muungano kuna uwezekano wa baadhi ya sehemu kudai kujitenga baada ya tanganyika kubaki peke yake au ukabila ukamea na kuota mizizi katika taifa letu. Kwahiyo mtawala atakayetawala Tanganyika lazima atapata tabu kuviweka hivi vipande pamoja. Wanaodai tanganyika ni watu wajinga au wanadhamira mbaya ya kuua utaifa wetu. Hakuna kitu kitakachobaki kinachoitwa Tanganyika baada ya kujitoa kwenye muungano. Ni marufuku kuirudia Tanganyika. Tukirudi nyuma madhara tutakayokumbana nayo tutajuta.
 
Tawala ndogo ndogo za kama kabila.
 

Man what have you been smoking? What the Germans did was to create a geographic area. However, that is only one attribute of the nation. Other attributes are people, languages, and traditions. These three are the results of our own existence. More importantly, they are bigger than the geographic area that the Germans left. So you can't say Tanganyika isn't a nation or it can't survive on its own.
 
Zakumi jaribu kujenga hoja bila kutukana hii peke yake Inaonyesha udhaifu wako katika fikra.
 
Zakumi jaribu kujenga hoja bila kutukana hii peke yake Inaonyesha udhaifu wako katika fikra.

You insulted me first and I am just reacting. In your introduction you say "Any intelligent Man will honor Mwalimu Julius Kambarage Nyerere for the creation of Tanzania"

Personally I don't honor Nyerere for the creation of Tanzania. Who am I? According to you I am an not intelligent man. That hurts my feelings.
 
Naomba ufafanuzi kidogo inakuwaje watu wale wale wabadilike kutokana jina tu? yaani tukibadilisha Tanzania kuwa Tanganyika basi kutakuwa na ukabila ni kitu gani kilichomo ndani ya Tanzania ambacho kinazuia ukabila?


Katia haya yako ya mwisho unasema "Tanganyika haikuundwa na dhamira yetu... je neno Tanzania limetokana na nini?
 
Nadhani Alinda majibu yapo Kwenye andiko lenyewe. Labda niliuze tunaitaka Tanganyika kwasababu gani?
 
Sikuona majibu na ndo maana nikakuuliza, Hivyo basi mtu anapouliza inamaana ulichoeleza hajakielewa/ au kama amekielewa anahitaji maelezo zaidi...
 
Kabla ya Mkoloni enzi za Romans, nchi yetu ikiitwa Azania na eneo lilikuwa kubwa nadhani toka Kenya hadi South..Tanganyika ilikuwa ni pamoja na Rwanda na Burundi, sasa tukiidai Tanganyika inabidi tuzidai hata Rwanda na Burundi maana tutakuwa na haki nazo.
 
Kwangu mimi ni vigumu kuamini Kitu kama hiko kutokana na mambo kadhaa ya kimsingi. La kwanza ni uwezo wa watu watu wa wakati huo kuendesha na kutawala eneo kubwa kama hilo. Hawakuwa na uwezo wa kuendesha kitu complex kama nchi. Hawakuwa na uwezo wa ku organize na kuunda nchi. Hizo ni myth tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…