Our Tax Man is a Brutal King

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Kwanza nimetumia style ya kibongo muvi kuandika taito ya kizungu alafu habari yenyewe ya Kiswahili ili kuwatisha waliokimbia umande!
Ninawashangaa watu wanahangaika na Ukawa, huku wakimuacha tax man wetu akijipandishia mikodi vile anavyojisikia.
tax man wetu anafananishwa na mfalme katili asiye na huruma kwa wananchi wake! Staili anayotumia ni bora punda afe ila mzigo ufike.
Hivi umeshawahi kuwaza kuwa nchi tajiri duniani zenye watu tajiri wanalipa kodi ya mauzo (Vat) ya 6% na hivi majuzi huko Japani wamepandishiwa kufikia 7% ya Vat na watu wamesusia bidhaa. Huku kwetu tax man wetu ana axe 18% kwa mtanzania masikini ambaye hata kununua mafuta ya taa lita moja ni shida.

Hivi unajua kwa nini tax man wetu amekuwa mkatili kiasi hicho? Ni kwa sababu hakuna umoja wa walaji (Consumerism) na angalau wale ambao wangetutetea ndio kwanza wako kwenye ukawa.
Masikini umejitahidi ununue kagari chakavu maana umechoka kuning'inia kwenye dala dala, ukikafikisha hapa tax man anakuadhibu kwa kuchafua mazingira. Kweli umasikini ni kichefu chefu! Eti unachafua mazingira. Kwa hiyo watakuadhibu kwa kukuwekea mikodi lukuki mpaka unapatwa na kifafa! Yani ni shida.
Mimi sina cha kumfanya tax man wetu. Ninachokifanya ni kumkabidhi mikononi mwa Mungu na kumuombea aokoke siku moja ili apate hofu ya Mungu na kuweza kuwahurumia wananchi maskini. Ipo siku ukatili wa tax man wetu utafika mwisho tu. Hilo naamini hivyo.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…