Unafikiri kwanini kuna nchi zimeendelea mpaka kuweza kutulemaza sisi kwa kutegemea misaada yao? Unafikiri wananchi wao wana simile na viongozi?? Jinsi Waafrika tulivyo na tamaa na kujawa ujinga mwingi, tusipoamka sasa hivi na kuwakomalia hawa wanaochukua fomu na kuomba kutuongoza unafikiri tutafikia hata nusu ya matamanio yetu??
Pamoja na mafanikio yake ya kuhesabika kwenye baadhi ya mambo, ukweli unabakia palepale, Mh. Rais wetu ni bitoo fulani hivi na anapenda kukata mbuga kichizi, jambo ambalo si baya hata kidogo kwa mtu binafsi tu au mfanyabiashara fulani hivi. Ila tatizo na manung'uniko mengi yanatokana na cheo cha huyu ndugu yetu na mzazi; Ni Mh. Rais wa Jamhuri ya Tz! Tunamhitaji nyumbani. Sote tukiamua kukaa kimya, hachelewi kufunga safari za miezi 3 au 6 Thailand bila kugeuza home. oooh hoh!