Over 1.2 million jobs created

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Over 1.2 million jobs created

DAILY NEWS Reporter

Daily News; Sunday,January 18, 2009 @21:15


(a) Are these figures correct?

(b) How many jobs were promised per year?
 
Kampeni za 2010 zimeanza. Tunataka breakdown ya kuonyesha sekta mbali mbali zilizoongeza ajira tangu 2005 hadi sasa, kila mkoa umeongeza ajira ngapi, kila kampuni au shirika limeongeza ajira ngapi. Pia tunataka independent entity kama Ernst and Young wapewe kazi ya kupitia rekodi zote kuhusiana na ajira toka December 2005 hadi sasa ili watuthibitishie kwamba kweli ajira 1.2 million zimeongezeka nchini tangu wakati huo hadi sasa. Hatuiamini hii serikali na mfano mzuri ni kushindwa kuthibitisha wapi zilipo pesa za EPA na kutoa majina ya wote waliorudisha na kiasi walichorudisha zilizorudishwa zinazodaiwa kufikia bilioni 69. Bila independent entity kututhibishia ajira hizo basi huu ni uwongo mtupu!!!!
 
Kazi hewa hizo wakuu. Hivi huyu waziri kweli anajua maana ya watu 1.27 kupata kazi?

Mambo mengine yanatia kichefu chefu kweli kweli.
 
A sensible politician would atleast go on the record as saying that due to the recent economical downturn the ambitious amount of creating a million jobs would have to be deflated to atleast 400,000.. lakini according to bogus massaged figures Kikwetes Government has managed to exceed excpectation even durin a global economic Slowdown....Wadanganyikwa Oyeeee!!!!
 
Mama Ntilie, Machingas na wauzaji wadogo wadogo wanazidi kujikomboa. Jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu, wananchi kama hawa inabidi watafute njia yeyote ya kuishi.

Hizo namba anazojumlisha waziri, zilikuwepo toka hata JK alivyosema ataleta ajira milioni moja. Uchumi wa nchi nyingine unaporomoka, sisi tumeweza kuleta kazi milioni 1.2,

1 - Je uchumi umekuwa sambamba na ongezeko la ajira?
2 - Je hali ya mwananchi imekuwa bora kutokana na ajira?
3 - Je huduma zinzotolewa kwa wananchi zimeboreshwa?
4 - Je kodi kutoka kwa haya makampuni yanayofanya vizuri ilikuwa kiasi gani kutokana kukua kwa hizo kampuni?
 
....nafikiri huyo waziri ni mwendawazimu!
 

Kapuya anatufanya watanzania wote ni vilaza; je hiyo informal sector anayozungumza ni kitu gani? Je ni pamoja na machinga na akina mama nitilie? Je ndizo ajira zilizoahidiwa na Rais? Kwa nini asiwe explicit na kutoa mchanganua wa hiyo informal sector na kutuambia alikopata takwimu za machinga na mama ntilie?
 
Mwakaa 2005 wanachama woote wa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania walikuwa hawafiki milioni? Well swali rahisi kwa kapuya.......... Wamejiunga wanachama wangapi wapya into that period katk NSSF, PPF, LAPF n.k?
 
Ni huyu Kapuya aliyekoroga mambo katika wizara ya elimu.....Sometimes huwa nawatizama wanasiasa wa bongo(baadhi) kama suicide bombers!!!
 
Pia ionekane nini jitahada gani zimefanyika ili ajira kupatikana. kuna ajira za machinga na mama Ntilie ambao wamekuwa wakipigwa vita ila wamejiajiri kwa nguvu zao na jitihada bila msaada wowote wa serikali au taasisi yoyote.

watoe mchanganuo unaweza kueleweka sio hizo blah blah zinazoendeshwa na siasa tu. Nadhani ni gia no.1 ya 2010
 
.....Sometimes huwa nawatizama wanasiasa wa bongo(baadhi) kama suicide bombers!!!

Ni huyu Kapuya aliyekoroga mambo katika wizaraya elimu kuna jamaa aliwahi kuninong'oneza kuwa huyu jamaa ni dizaini ya yule waziri aliyefuta michepuo ya kilimo na sayansi mashuleni...Mu...ngai.alivurunda hata wizara ya washika bunduki and was so mlafi9alitumia hata hell-co-opter ya washika bunduki for private safaris.
lakini upande wa pili ni kweli ajira zimeongezeka siwenyewe mmesikia au kusoma ktk media kuwa kuna vijana wamejiajiri kwa majina tofauti-tofauti.Mfano Mtwara wapo TUKALE WAPI, Dar ndiyo zaidi kama vile MBWA MWITU(mbagala-mtoni),Squad(Tandika)janjawid(jangwani) nimesahau majina ya wale wa manzese,kigilagila,tandale,n.k. Arusha wapo ngaramtoni,unga limited, nk.Mwanza wapo mwaloni
 
Mawaziri wanajua bosi wao anataka asikie nini kutoka kwao. Tungekuwa na upinzani mzuri kama ule wa David Cameron na Gordon Brown taarifa za namna hii zisingekuwepo.
 
Wakati wa bajeti alisema kuwa serikali ilikuwa imetengeneza ajira laki nne unusu tu. Ina maana kati ya Julai mwaka jana na sasa zimetengenezwa ajira takriban laki nane... najihisi niko nchi ya KUFIKIRIKA
 
Mungu Ibariki Tanzania kwa kweli. Na tudumishe uhuru na umoja. ila ipo siku...
 
Cant believe these figures and analysis are coming from a professor!!? How could Tanzania have 1.27 new jobs created within such a short time? Haya ndo mambo ya kupika data.... you start from the answer going back!!
 
Duh;

Professor Kapuya katoa data; hawa ndio wale wasomi wanaosifwa na baadhi ya watu kwa kuwalinganisha na walioishia form four na six... sawa bana!

Sijui na waliopoteza kazi ni kiasi gani, wanaosubiri ni kiasi gani na sijui ni mbinu gani zimetumika kupambanua informal sector

Maybe, ili atoe taarifa bora yenye upembuzi yakinifu, its worth kusema kwamba kiongozi huyo kaongea utumbo na asirudie tena sweeping statements
 
Last edited:
Ndio inaweza kuwa hiyo figure ni kweli but wengi waliopata hiyo ajira ni
Walimu wa CRUSH PROGRAM-miezi 3
Askari POLISI
Askari JWTZ & JKT
Askari MAGEREZA
 
Hawa wanafikiri watanzania hawana akiri hata kidogo, wanaficha uongo wao kwenye informal sector wakiju kuwa watu hawawezi kufuatilia wakati ambao informal sector imepoteza wafanyakazi zaidi wao ndio wanaficha uongo wao huko.

wamachinga wangapi wamerudi kwao kwa kukosa sehemu za kufanyia kazi, viwanda vidogo vidogo vingapi vimefunguliwa, maduka mangapi yamefungwa. inabidi watupe data za aina hii watuambie jinsi wanavyokusanya data zao na sio bla bla zao
 
....nafikiri huyo waziri ni mwendawazimu!

Ulitegemea nini kipya kutoka kwa Mh. Waziri, wakati JK mwenyewe alisaula bungeni kwa kusema wabunge wameongeza ajira za MAHAUSIGELI ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…