Overconfidence itaiponza Yanga kesho

mjogoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
882
Reaction score
652
Kwa miaka ya hivi karibuni Yanga wamekuwa wakiingia kwenye hizi mechi za watani wakiwa underdog. Hiyo inasemwa kuwa ilichanjia wao kupambana sana na hata kupata matokeo mazuri (kutofungwa) kwa karibu misimu mitatu.

Hata hivyo, hali imebadilika sana. Yanga wanajiona wana timu yenye ushindani na wameanza kujiamini sana. Kwa mtazamo wangu, hali hii ya kujiamini sana inaweza kuwaponza ktk mechi ya kesho dhidi ya Simba (anayetaka japo kuwapoza mashabiki wake kufuatia machungu wanayopitia).

Mwenzangu unaonaje?
 
Kwamba Yanga wanajiona wana team kumbe hawana si ndio?
 
Binafsi mm nafuatilia sana hizi timu. Ila Yanga inapokuwa vizuri huwa ni ngumu sana kupoteza kwa Simba. Yaan Katika mechi 10 ambazo Yanga wanaonekana bora basi watapoteza 2 na 2 draw na hizo 6 SIMBA anakufa.

Yanga wakiwa kwenye form hawana kudharau mechi, tatizo la Simba wakiwa kwenye form ndio hucheza as if hawana haraka na Goli.

Ushauri wangu kwa Simba wacheze kwa jihadi sana, striking force ya Yanga ni hatari mno hasa kwa beki kama Kapombe, Hussein na Onyango ambao kwao Speed ya kuzuia ni ngumu.

Kuna kila dalili kesho kiungo wa Simba akala umeme, kwa jinsi navyoona vikosi vyao ni rahisi mno kucheza rafu za kizembe.

Pia kwa Yanga Bangala ni mwepesi kucheza Rafu hivyo kwa usumbufu wa Morrison itampa shida sana.

Kiujumla mechi inatabirika mno,
FT YANGA 3-1 SIMBA.

Mechi hii kwa asilimia kubwa imechezwa nje ya UWANJA hasa ZANZIBAR na BAGAMOYO.
 
KOSI limeshiba hakuna cha overconfidence wala nini, Quality itaamua..kocha wetu ameshawaandaa wachezaji kisaikolojia

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Inonga aiku yake ya kupata red imefika
Ashindwe kupata kadi kwenye mechi ngumu za kimataifa na nyingine hadi zilikuwa na VAR, aje apete akiwa anacheza na domestic team?

Ile game waliyokaba kwanzo mwisho kule kwa madiba hakupata kadi, kadi aje aipate leo kwa hawa wasaga sumu?
 
Ulivomalizia daaah
 
Wasaga sumu!!! Una mbwembwe sana
Ashindwe kupata kadi kwenye mechi ngumu za kimataifa na nyingine hadi zilikuwa na VAR, aje apete akiwa anacheza na domestic team?

Ile game waliyokaba kwanzo mwisho kule kwa madiba hakupata kadi, kadi aje aipate leo kwa hawa wasaga sumu?
 
Ashindwe kupata kadi kwenye mechi ngumu za kimataifa na nyingine hadi zilikuwa na VAR, aje apete akiwa anacheza na domestic team?

Ile game waliyokaba kwanzo mwisho kule kwa madiba hakupata kadi, kadi aje aipate leo kwa hawa wasaga sumu?
Game ya Geita alipewa red card ilikua international?
 
Sikumbuki ni lini mara ya mwisho yanga alimfunga Simba kwa aggregate hiyo.
Wakuu nikumbusheni?
 
Mambo ya kichawi achana nayo ni kupoteza muda wako tu , last time mlikuja hapa Yanga anapigwa 3-0 ngao ila Yanga akashinda 1-0 ,yaani ongea point zako tu sio habari za ushirikina
 
Sijui kama una elewa maana ya Aggregate.
Simba 0 - 2 Yanga
Yanga 2 - 0 Simba

Vipi hapo inafanana na mantiki yako au
Ok, nilichomaanisha yanga hawezi mzidi Simba 2 more goals.
Tabiri zenu ziwe Yanga 1 - 0 Simba, sio hizo ndoto za yanga 3 - 1Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…