apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Ndugu wanajamvi kweli ule usemi wa ukitaka kujua shida ziko wapi nenda hospitalini(za serikali), mahakama na polisi.Hali iliyopo Oysterbay polisi ni zaidi ya huko kote.
Binafsi nilipata fursa ya kufika hapo baada ya kupata ajali (nikiwa gari yangu imegongwa na mgongaji uwezo mdogo hivyo kuhitaji Bima yake itibu gari yangu).Cha kushangaza nilianza kuombwa rushwa kuanzia Traffic eneo la tukio,vehicle inspector,mfungua file,mpiga chapa na mpelelezi (wote traffic hawa).
Mazee mkono umekuwa mfupi mpaka sasa kesi yangu haieleweki japo hajafa wala kujeruhiwa mtu kwenye ajali hiyo.Kila nikienda file halionekani, nikamtafuta mgongaji wangu (Dreva ambaye hayuko vizuri kimapato) akadai hata yeye anashangaa kwa nini hawajamfikisha mahakamani wakati kila kitu kimezingatiwa.Alidai jamaa walimwambia akitaka mambo yaende haraka ''akunjuke''.
Kuna kichwa kinaitwa Ambwene, du! Yaani utadhani nchi haina mtu, yaani anakwambia kabisa uandae cha kwake kabla hajafanya inspection.Binafsi nimepata mshituko, huyu mtu amedumuje hapo na kujiachia kihivyo.
Kwa ujumla afya zao ni nzuri, vijiti mdomoni na wala hawana wasiwasi.WanaJF ebu nipeni ushauri jinsi ya kutatua hiyo issue yangu.
Tupo pamoja.