P-Funk alizikonga roho zetu

P-Funk alizikonga roho zetu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
NAJILIPUA
NI kweli ni trend- setter na alitengeneza top ten lakini kwa upande wangu, midundo mitano ninayoielewa zaidi kutoka kwake ni hii;

1. MTOTO WA KIUME - GEEZ MABOVU
Dundo linaanza, landlover linatekenywa kisha dundo linaanza taratibu na ule msauti mzito wa Geez na vile anavyopita kama hataki, basi kwangu ni burudani tosha.

Jumlisha na namna mtoto wa kiume alivyochorwa humo, siyo watoto wa kiume wa "sponsor niachie my wangu"

2. MOTO WA TIPA - ZOLA D

Unde mzee wa ngumi kila sekunde alipita sana humu, ubabe mwingi na tambo za kutosha. Akiwasha Nani wa kuzima? Labda apande pipa.
Bonge la dundo lilikutana na bonge la voko.

3. MSTARI WA MBELE - KALA PINA
Ile intro kwanza; " mananta! Mananta! Man shmuka! Kuna Kiarabu hapo na Masoud anaappreciate kwamba ni bonge la beat.

Tambo na punches kibao halafu tofauti na ngoma zilivyozoeleka, hii ina transition ya beat na Pina anaswitch flow Kisha inaingia Chorus
Kuna Ile outro sasa, sauti ya mkwaruzo ya Pina, halafu anabadili sauti na kusema " ee bwana noma" na ilikuwa noma kweli.

4. TUNASONGA - PINA NA DOGO
Bonge la majibizano humo kutoka kwa wana Kikosi.
Pina anasema hili beat halikufanyiwa mixing wala mastering, P akawazingua, wakainyonya kwenye CD na kwenda kuitambulisha redioni mpaka kusambaa mtaa.

Pata picha ingekamilika ingekuwaje?

5. RATIBA ZETU- SNA LEE FT NGWEA
P alitengeneza beats nyingi sana za kuruka kwanja lakini kwangu hii ni bora zaidi.

Snoop Lee sasa alivyoichambua wiki nzima humo. NI LAANA

BONUS;
PEKE YANGU - ADILI
HAWATUWEZI - N2N FT ENIKAH
NINI MNATAKA - PIG BLACK
NIPE TOP FIVE YAKO KUTOKA KWA P.
341343023_1184204912981184_6317377537102673949_n.jpg
 
Elimu dunia
Nipe tano
Mzee wa busara
Darubini kali
 
Da respect Sana mwana umeua Sana kiukweli imenikonga Sana Moyo wangu na kunikumbusha enzi hizo muziki ulipokua muziki....
Kwanza hizo Ngoma zote ninazo na hua nazisikiliza Sana...

Ila kwangu Ngoma tano ambazo majani alitisha ni hizi...

05. NAMPENDA YEYE BY MH. TEMBA
Hili beat hua nikisikiliza naona majani alikua kwenye ubora wake kama ni Messi basi ni Yule wa msimu wa 2014. Kwanza beat Linaanza Majaniiii Temba hapa. Da na huyo demu alivoliwa kimasikhara ni shida..!

04. MWANZA MWANZA BY FID Q
Hii Ngoma ilitoka nakaribia kumaliza shule ya msingi nakumbuka siku za ijumaa nilikua siendi shuleni ili niisikilize kwenye top ten za RFA... Aisee hapa majani alikua heaven.

03. JIACHIE CHIDI BEENZ
Humu kuna matusi makubwa majani alifanya maana sio poa, Beat lilikua linaitikia lenyewe nheeenti...
Dah! R.I.P maunda Zoro huyu dada aliua sana kwenye chorus
Baada ya hapo CHIDI alipata umaarufu mkubwa sana

02. KISA DEMU BY JUMA NATURE
Juma Nature msanii aliyekua na vibe lake. Sasa kwenye hii Ngoma walikuatana mafundi.

01. WANAPAGAWA BY JEBI
apumzike Kwa Amani Jebi. Kuna kale kamstari anasema
"Napenda dancehall ila siwezi tu ku-shake, midundo ya Sean Paul inavopigwa tu Kwa chati... Da hatari sana
 
Wanapagawa ni mkono wa Bonny Luv, sio Majani.
 
Bila unafiki kwa P siwez kuchagua beat ipi kali,
Zote zilikuwa moto[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Umesahau Msamaha wa Kajala mzee.

Please 4give Him...!
 
Back
Top Bottom