PAC yazitimua taasisi mbili za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imezitimua kwenye kikao taasisi mbili zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi baada ya maofisa masuhuli kushindwa kufika kwenye kikao hicho.

Taasisi hizo ni Wakala wa Barabara Nchini (Tanroad) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), ambazo zilifanyiwa ukaguzi maalum na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza leo Jumanne Januari 17, 2023, Mwenyekiti wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka amesema taasisi hizo zimekuwa matatizo makubwa ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakijirudia rudia.

Amesema ukaguzi huo ulifanyika kwa hesabu za miaka mitano za taasisi hizo kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, ulilenga ni kubaini fedha zilizopotea kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo mikataba mibovu.

Hata hivyo, Kaboyoka amesema aliyefika mbele ya kamati hiyo alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi tu ambaye kisheria siyo ofisa masuhuli anayetakiwa kuwajibika kisheria mbele ya kamati hiyo.

Amesema katika kipindi hiki walitaka kufanya tathmini kuona ni kiasi gani cha fedha kimepotea chini ya wizara hii na akashauri ifike mahali kufanyike mabadiliko ya jumla ya watu wanaochezea fedha za umma kwenye taasisi hizo.

“Tunaomba mwenye mamlaka ya kuchukua hatua achukue hatua. Haya mambo yamekuwa yakijirudia. Pia sisi tunasikia huko mtaani wanasema Bunge si kazi yake kutoa mapendekezo maazimio na kelele hawa ni wasiasa wamezoe kupiga kelele,” amesema.

Kaboyoka amesema taasisi hizo zimekuwa zikifanya kazi kwa mazoea na hivyo leo kamati hiyo imesema haiwezi kupoteza muda wa kuzungumza nao.

“Kuwauliza maswali yale yale, majibu yale yale na matendo hamna,”amesema Kaboyoka baada ya kuwaondoa katika kikao hicho viongozi wa taasisi hizo walioambatana na Naibu Katibu Mkuu wa sekta ya ujenzi.

Aidha, Kaboyoka amesema kamati hiyo haioni haja ya kuwaita tena katika vikao bali wataandaa ripoti yao na kupeleka ndani ya Bunge ili liamue maana haliwezi kuendelea kudharauliwa.

Mwananchi
 
Tanroads ni mrija wa kupitishia wizi wa pesa za umma. Awamu ya 5 kulikuwa na wizi mkubwa kupindukia lakini taarifa zake zilidhibitiwa na watawala.

Musa Asad aliondolewa kwenye nafasi yake kama CAG kinyume cha katiba kwa sababu alikuwa anataka kuanika wizi uliokuwa unafanywa.
 
Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imezitimua kwenye kikao taasisi mbili zilizoko chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi baada ya maofisa masuhuli kushindwa kufika kwenye kikao hicho.

Taasisi hizo ni Wakala wa Barabara Nchini (Tanroad) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), ambazo zilifanyiwa ukaguzi maalum na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza leo Jumanne Januari 17, 2023, Mwenyekiti wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka amesema taasisi hizo zimekuwa matatizo makubwa ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakijirudia rudia.

Amesema ukaguzi huo ulifanyika kwa hesabu za miaka mitano za taasisi hizo kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, ulilenga ni kubaini fedha zilizopotea kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo mikataba mibovu.

Hata hivyo, Kaboyoka amesema aliyefika mbele ya kamati hiyo alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi tu ambaye kisheria siyo ofisa masuhuli anayetakiwa kuwajibika kisheria mbele ya kamati hiyo.

Amesema katika kipindi hiki walitaka kufanya tathmini kuona ni kiasi gani cha fedha kimepotea chini ya wizara hii na akashauri ifike mahali kufanyike mabadiliko ya jumla ya watu wanaochezea fedha za umma kwenye taasisi hizo.

“Tunaomba mwenye mamlaka ya kuchukua hatua achukue hatua. Haya mambo yamekuwa yakijirudia. Pia sisi tunasikia huko mtaani wanasema Bunge si kazi yake kutoa mapendekezo maazimio na kelele hawa ni wasiasa wamezoe kupiga kelele,” amesema.

Kaboyoka amesema taasisi hizo zimekuwa zikifanya kazi kwa mazoea na hivyo leo kamati hiyo imesema haiwezi kupoteza muda wa kuzungumza nao.

“Kuwauliza maswali yale yale, majibu yale yale na matendo hamna,”amesema Kaboyoka baada ya kuwaondoa katika kikao hicho viongozi wa taasisi hizo walioambatana na Naibu Katibu Mkuu wa sekta ya ujenzi.

Aidha, Kaboyoka amesema kamati hiyo haioni haja ya kuwaita tena katika vikao bali wataandaa ripoti yao na kupeleka ndani ya Bunge ili liamue maana haliwezi kuendelea kudharauliwa.

Mwananchi
wabunge wanajidhalilisha wenyewe ndo maana hata watendaji wameamua kuwadharau.
 
Back
Top Bottom