Padre 'ajilipua' kwa askofu Mwamakula kuhusu "Matembezi ya hiari"

Mbona humzungumzii Gwajima & the like? Hii hoja uliyokuja nayo sasa nimeshughulika nayo sana tu. Binafsi siungi mkonop watumishi wa Mungu wakati huo huo wanakuwa wanasiasa wa moja kwa moja huku wakisimaam madhabahuni kama wachunga kondoo, najua wanafanya usanii tu. Na mfano ni Gwajima. Nimetofautiana na wewe unapotaka kuonyesha kwamba viongozi wa dini wanapaswa kubaki kimya na kuachia wanasiasa wafanye upuuzi, na ukatoa mfano wa huyo "mtaalamu mmoja". Hilo nalipinga! Kufanya checks & balance kwa viongozi wa dini ni sehemu ya injili kama utapenda kuelewa leo.
 
Dhambi ziko nyingi mno sio moja.ukisema tubuni na kuiamini injili umemaliza kila dhambi aliyonayo mtu badala ya kuhubiri dhambi moja moja!!!! Narudia kazi ya Askofu ni kuhubiri watu watubu na kuiamini injili awe Mwamakula, Gwajima,Kakobe Papa au yeyote

Watu wakitubu na kuiamini injili mambo yote yatakaa vizuri iwe kwenye siasa sijui katiba sijui nini kutanyooka bila watu kutubu na kuiamini injili mambo mengi hayatakuwa sawa!!
 
Kwahiyo hizi picha zinajibu swali la wkamba Mtikila aliuawa? Mleta uzi amechota kilichoandikwa na Askofu Mwamakula kama kilivyo akakileta kwenye hili jukwaa ili members wajadili kama ilivyo kawaida, sasa unamuwakia kwanini? kosa lake ni nini?
 
Mwamakula kusimama na kuhamasisha watu wadai TUme Huru na Katiba mpya ni sehemu ya injili, kama unataka kuelewa kuanzia leo elewa. Ungekuwa umesoma theolojia vizuri usingepata shida kuelewa!
 
Mwamakula kusimama na kuhamasisha watu wadai TUme Huru na Katiba mpya ni sehemu ya injili, kama unataka kuelewa kuanzia leo elewa. Ungekuwa umesoma theolojia vizuri usingepata shida kuelewa!
Mwamakula sio askofu huyo ni mwanaharakati wa kidini kama walivyo wengine duniani. Wajikite katika TIBA ya ROHO hayo mahitaji mengine ya nafsi na mwili yatarekebika kutokana na watu kuwa na mioyo ya unyoofu, kutenda mema na haki ikiwa pamoja na serikali maana inaongozwa na watu wenye nafsi, mwili na roho. Viongozi wa kidini ambao kutwa kucha ni kuzua fikra chonganishi watatoa hesabu ya matendo yao mbele za mwenyenzi Mungu aliye hai. Kutetea haki za watu za kidunia hazihesabiki kutakasa roho inayokubalika na Mungu.
 
Sio kweli. Mitume na manabii wali
 
Yawezekana hujui maana ya kuchapa kazi ? Uchape kazi gani hakuna Ajira bodi ya mikopo ni kama ulivyosikia.
 
Sijaelewa kidogo.... usintamaze lina maana gani.

Ila nadhani anamtahadhalisha kuwa Mtikila, Mchungaji marehemu alikufa/aliuawa kwa vile alikuwa anaipinga serikali... mihimili ilimshughulikai (ndivyo nilivyoelewa) I stand to be corrected
Wakuu msitengeneze history mpya. Mtikila alikuwa anampinga kwa nguvu zote mgombea wa Ukawa na alipata ajali akiwa njiani anakuja Dar kufanya press conference.
 
Yawezekana hujui maana ya kuchapa kazi ? Uchape kazi gani hakuna Ajira bodi ya mikopo ni kama ulivyosikia.
Ajira gani unazosema hazipo ?
Tanzania ina fulsa lukuki.
Fulsa za Bahari.
Fursa za Ardhi yenye rutuba tele na maji ya kutosha.
Fursa za Anga.
Wahamasisheni vijana wenu wapende Masomo ya Ufundi ya Veta ambako kuna fani nyingi mno zinazotoa ajira mara baada ya kuhitimu.
Mfano, Useremala.
Sasa hivi Seremala wa Keko Fenicha wanauza fanicha nyingi sana Nchini Visiwa Moritius.
Kila baada ya miezi miwili inakuja Meli toka Nchini humo na wafanyabishara wa huko wananunua karibu fanicha zote.
Wacha wateja wa ndani.
Mbao zipo za Kumwaga Nchi hii, wezi wote wa zamani wa Keko sasa hivi wanafanya kazi na wameacha wizi.
Tanzania Mbao za Kumwaga.

Huo ni Ufundi mmoja tu.
Waelimisheni vijana waache kudharau fani za Veta na kukimbilia kusoma Digree za Nadharia za Utawala, Ugavi, nk. Ambazo hazifundishi kujitegemea na ajira zake hazipo sawa na wingi wao.

Sasa hivi dili ni Masomo ya Veta.

Mnawapotezea Muda wao, Maandamano maandamano, huku mnawatumia kama ngazi za kupata madaraka ya Kisiasa halafu mnawatupilia mbali.

Hivi CHADEMA ingeshinda uchaguzi ingeweza Kuwaajiri Wahitimu wote wa nchi hii ?
Au nusu yake ?

Wacheni kuwapotezea Muda vijana.
 
Wewe unajihusisha na shughuli gani kati ya hizo ulizotaja? Nchi imepata uhuru miongo Kazaa iliyopita ukienda hapo RUFIJI TU barabara hazina lami ni tope hasa wakati wa mvua hayo mazao utapitisha wapiiii
 
Mwamakula kusimama na kuhamasisha watu wadai TUme Huru na Katiba mpya ni sehemu ya injili, kama unataka kuelewa kuanzia leo elewa. Ungekuwa umesoma theolojia vizuri usingepata shida kuelewa!
Theolojia ni elimu ya kuhusu Mungu sio wanadamu!!! Is the study about God Not about people people!!!! Hizo study about people waachie wataalamu wa biolojia,siasa na wanaharakati

Rudi kasome tena hiyo theolojia yako koko
 
Wewe unajihusisha na shughuli gani kati ya hizo ulizotaja? Nchi imepata uhuru miongo Kazaa iliyopita ukienda hapo RUFIJI TU barabara hazina lami ni tope hasa wakati wa mvua hayo mazao utapitisha wapiiii
Wakati wa mvua huwa ni wa kulima sio kusafirisha mazao wewe vipi? Akili huna

mazao unasafirisha kipindi ambacho ni kiangazi kipindi ambacho hakuna tope.
 
Wakati wa mvua huwa ni wa kulima sio kusafirisha mazao wewe vipi? Akili huna

mazao unasafirisha kipindi ambacho ni kiangazi kipindi ambacho hakuna tope.
Wawapi wewe???? KOROSHO zinavunwa mwezi wa kumi hadi December hakuna mvua kipindi hicho????
 
Wawapi wewe???? KOROSHO zinavunwa mwezi wa kumi hadi December hakuna mvua kipindi hicho????
SEhemu zinakovunwa ardhi ni ya mchanga huwezi kutana na tope.Sehemu zenye tope mikorosho haistawi
 
SEhemu zinakovunwa ardhi ni ya mchanga huwezi kutana na tope.Sehemu zenye tope mikorosho haistawi
Nenda MKURANGA kijiji kinaitwa magawa acha kubishana ujinga! Pita barabara ya nyamisati acha kubishana ujinga
 
Mchungaji marehemu alikufa/aliuawa kwa vile alikuwa anaipinga serikali... mihimili ilimshughulikai
Timing ya kifo inapingana na dhana ya kuuliwa na serikali. Aliuliwa na mmoja wa wasaka urais.

Hatujasahau kuwa hata mzee Kasoli alilazimika kukimbia makazi yake huko Arusha baada ya kutishiwa kifo na wasaidizi wa mgombea wenu 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…