Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Mwanzoni kabisa mwa 2000, Pep Guardiola na rafiki yake wa karibu Gabriel Batistuta walikuwa wanapiga stori kwenye viwanja vya mazoezi vya AS Roma baada ya mazoezi mazito, wakizijadili ndoto zao baada ya kustaafu soka, Batistuta alikuwa na ndoto ya kuruka viwanja kuanzia Ibiza Spain mpaka Mykonos Ugiriki
Guardiola ilikuwa tofauti kwake, aliwambia rafiki yake ndoto zake za kuwa Kocha mkubwa wa soka duniani, Batistuta bila kinyongo akamwambia "Kuna Mzee mmoja anapatikana maili 3,188 kutoka hapa tulipo, huko nyumbani Buenos Aires Argentina, anaitwa Marcelo Bielsa nenda kaongee nae"
Ilipita muda baada ya majadiliano yao, Batistuta yupo zake Mykonos anakula bata, Pep Guardiola anapanda ndege Barcelona kuelekea Argentina safari ya masaa kama 13 angani, kila mtu kati yao anaelekea kutimizia ndoto zake baada ya kustaafu soka, Pep anaenda kuonana na mtu ambaye hana uhakika atampokea vipi
Wakati anatua uwanja wa ndege, aliongoza moja kwa moja kwa Mwalimu Bielsa, alipofika nyumbani hakuonana na Bielsa bali mkewe tu "Mzee nimemkuta?" Mama alimwambia hayupo ila nenda na huyu mdogo wako atakufikisha shambani kwake, Pep aliongozana na Demetrio mpaka kwenye ranch moja
Huko ndipo alikutana na Bielsa, Mzee mmoja aliebeba tumaini lake kubwa kwenye dunia ya Ukocha, walisalimiana na Bielsa alimpokea kwa furaha sana, na kwakua wote wanazungumzia Kihispania walielewana vyema, ikumbukwe Bielsa anajua lugha moja tu, lilianza darasa la masaa 11 ya kuongelea soka sasa
Guardiola anakiri kwa kinywa chake kuwa, waliichambua mifumo zaidi ya 10, walijadili mbinu zaidi ya 100, walizichambua timu zaidi ya 100, ubaya zaidi Bielsa alikuwa anamchambulia kila Kocha na madhaifu yake huko Ulaya, walikunywa chai ya asubuhi shambani, chakula cha mchana shambani na chakula cha usiku shambani
Guardiola alimuuliza kwanini anamfundisha yote hayo?? Bielsa alimwambia "Mwalimu anaweza kukufundisha kila kitu na bado akakupa mtihani ukakosa na Mwalimu anaweza kufeli mtihani wako kwa vile alivyokufundisha kama utamtungia wewe" alijibu tu kimafumbo ila alimaamisha kuwa siku wakionana tena awe ameiva
Bielsa alichukua makaratasi na kuanza kumchorea baadhi ya vitu muhimu sana kutoka kwa Makocha mbalimbali, alimwambia kila kitu kuhusu Arrigo Sachi, Carlo Ancelotti, Mircea Lucescu wa Shakhtar Donetsk na Marcelo Lippi
Baadae akamwambia
"Mwanangu mimi ni Mzazi, nimewafundisha vijana wawili kuna wewe na Diego Simeone, mtaamua wenyewe kuwa wachawi au kuwa malaika" alimwambia hivyo kwakuwa aliwapa kila kitu kuhusu soka la kujihami na kushambulia, uamuzi ni wao
Bielsa hapendi soka la kujilinda ndio maana anapenda kumuita Simeone shetani na Pep Malaika kwakuwa anafunguka, alimaliza somo lake na kurudi na kijana wake nyumbani kwake, asubuhi Pep aliaga na akakabidhiwa kitabu maalum (Ipo siku nitaelezea kitu hiki)
Kumbuka Pep alipewa ahadi kuwa siku wakikutana tena amkute ameiva na anacheza kama alivyomwambia, ahadi yao ilitimia walipokutana Spain, Pep yupo na Barcelona na Bielsa na Bilbao, walikutana mara tatu, Pep alishinda mbili na sare moja, Mwanafunzi aliiva sana
Kwanini watu wanamuita Bielsa Padre?? Kwa Kizungu wanamuita Priest of the Nun, hii ilitokana na baada ya kutimuliwa 2006 Ukocha Argentina akaamua akakae zake na Mapadre kutumikia tu jamii, hakutaka kujadili mpira kwa muda flani, ndipo hapo akapachikwa jina hilo
Kwasababu za Kiafya, Bielsa aliambiwa akae mbali na mpira ili atazame afya yake kuanzia 2015, akarejea nyumbani kwake Buenos Aires kwenye mji wa Pwani ya Kaskazini Mashariki, ndipo hapo ikaja Leeds United kuhitaji huduma yake ila hawakuwa wanaamini kama Legend atakubali
Simu ya Mmiliki wa Leeds, Adriazzini kuelekea kwa viongozi wa Victor Orta na Angus Kinnear iliwataka wasafiri mpaka Argentina kuonana na Mwalimu wa Pep baada ya Leeds kufanya vibaya 2017-18 Daraja la kwanza, baada ya Makocha wengi kufeli tu interview zao
Baada ya maili 7,000 walifika kwa Bielsa, ajabu wanakutana na Babu aliekuwa anawafahamu wachezaji wote wa Leeds, anaifahamu mifumo yote ya timu 20 za Championship, El Loco aliwaambia haitaji usajli mpya bali watoto walewale, baada ya misimu miwili katwaa ubingwa na kuirejesha Leeds EPL
Na huyo ndie El Loco Marcelo Bielsa, Mwalimu wa shetani na Malaika[emoji1666]