Nimesikitika kupewa taarifa ya kifo chake. Alikuwa mlezi wetu vijana pale Moshi wakati nasoma. Alikuwa anatoa semina kadhaa, mafundisho, anakuja maafari, tafrija na elimu ya dini.
Muda wake mwingi aliutumia kwa vijana ingawa sina hakika sana ila pia nakumbuka alikuwa anahusika na accounting za jimbo.
"Kwa kawaida ya binadamu mambo ya dini hayatuvutii, hatutakiwi kuendekeza starehe za dunia bali tutangulize ufalme wa Mungu" nukuu kutoka mojawapo ya matukio yake pale YCS tulipomaliza sherehe tukaweka mziki.
Aliporudi na gari kuchukua kitu alichosahau akashangaa kuona wanaocheza mziki ni wengi kuliko waliokuwa kwenye tukio. Alafu sasa wimbo wenyewe ulikuwa Tetema kipindi unatrend, kisha akatazama ambako tuliweka altare watu wanabambiana. Ila YCS tulikuwaga wahuni hadi CASFETA waligoma kutukodisha vyombo vyao eti tunavipigia nyimbo za kidunia.