Tabrett
JF-Expert Member
- Jun 5, 2013
- 522
- 338
Habari za jioni wanaJF,poleni kwa majukumu.Nimejaribu kufuatilia hizi pads tunazotumia akina dada nimegundua ziko za aina nyinginyingi zikitofautiana kwa muonekano,texture,hadi utendaji kazi wake.Kinachonitatiza hadi kuamua kuwashirikisha wanajukwaa ni kuwa,kumekuwepo na pads ambazo wanaozitengeneza wanadai kuwa zina dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kama fungus,kurekebisha mzunguko,UTI na wengine wameenda mbali zaidi kwa kudai zinatibu hadi ugumba.Wakati huo huo kuna minong'ono kuwa kuna pads nyingine zinasababisha cancer ya kizazi.
Hivi mwezi ulopita nilitembelea pharmacy moja nkapewa darasa kuhusu mzunguko na vitu vinavyoweza kuuathiri nkaelekezwa na pads zinazofaa kutumia na namna ya kuzitumia,kiukweli nilivutika nikazinunua na kuzitumia,kilichonishangaza ni kuwa yale maumivu ya tumbo yametoweka na mtiririko wa damu umepungua sana to the extent usiku nina uwezo wa kulala bila pad na nisiharibikiwe tofauti na awali ambapo ilikuwa ni maporomoko!Ndio nimeshuhudia matokeo chanya ila wasiwasi wangu ni kuwa je haiwezi kujaleta madhara hapo mbeleni?wenye utaalamu na uzoefu na hilo naomba wanitoe wasiwasi tafadhari.