Pads

Tabrett

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Posts
522
Reaction score
338
Habari za jioni wanaJF,poleni kwa majukumu.Nimejaribu kufuatilia hizi pads tunazotumia akina dada nimegundua ziko za aina nyinginyingi zikitofautiana kwa muonekano,texture,hadi utendaji kazi wake.Kinachonitatiza hadi kuamua kuwashirikisha wanajukwaa ni kuwa,kumekuwepo na pads ambazo wanaozitengeneza wanadai kuwa zina dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kama fungus,kurekebisha mzunguko,UTI na wengine wameenda mbali zaidi kwa kudai zinatibu hadi ugumba.Wakati huo huo kuna minong'ono kuwa kuna pads nyingine zinasababisha cancer ya kizazi.
Hivi mwezi ulopita nilitembelea pharmacy moja nkapewa darasa kuhusu mzunguko na vitu vinavyoweza kuuathiri nkaelekezwa na pads zinazofaa kutumia na namna ya kuzitumia,kiukweli nilivutika nikazinunua na kuzitumia,kilichonishangaza ni kuwa yale maumivu ya tumbo yametoweka na mtiririko wa damu umepungua sana to the extent usiku nina uwezo wa kulala bila pad na nisiharibikiwe tofauti na awali ambapo ilikuwa ni maporomoko!Ndio nimeshuhudia matokeo chanya ila wasiwasi wangu ni kuwa je haiwezi kujaleta madhara hapo mbeleni?wenye utaalamu na uzoefu na hilo naomba wanitoe wasiwasi tafadhari.
 

Zinaitwaje n ni sh ngap n zinapatikana wap?..In ma side sion kam zitakuwa na madhara.
 
Zinatengenezwa na World Great Herbs,zinaitwa Aloe Sanitary Napkins,bei nilinunua 5,000,kupatikana ni katika pharmacies.
 
Mh!haya makubwa sasa!kumbe kutoka damu nyingi nao ni ugonjwa?kwani kulikua na tofauti kati ya siku za mwanzo(wakati ndo unavunja ungo)na kipindi hiki kabla hujazitumia hizo pads?
 
Nenda na hizo pad kwa gyno
Sie hapa tutakuingiza machakani bure

Hivi kweli pad ziweze kata flow ndani ya mwezi mmoja huoni kuna tatizo???
 
Mh!haya makubwa sasa!kumbe kutoka damu nyingi nao ni ugonjwa?kwani kulikua na tofauti kati ya siku za mwanzo(wakati ndo unavunja ungo)na kipindi hiki kabla hujazitumia hizo pads?
Kwakweli mie sikunotice tofauti kati ya awali na hivi majuzi kabla ya kutumia,mi nilikua naona kama ni sawa tu,ila nilichokigundua ni baada ya kuzitumia ndipo maumivu ya tumbo na nyonga yalipokoma na damu(flow)imepungua sana kiasi nakuwa comfortable na kujisahau kabisa kama niko MP!
 
Nenda na hizo pad kwa gyno
Sie hapa tutakuingiza machakani bure

Hivi kweli pad ziweze kata flow ndani ya mwezi mmoja huoni kuna tatizo???
Hao magyno pia wanaaccount humu ndani thats why nimesema kwa mwenye utaalamu na hilo.
 
Mamii, kutoka damu ni natural na ina umuhimu wake. Kitu chochote chenye kuingilia natural process ni hatari kwa afya yako. Sikushauri kupata tiba ya kwenye pads unless umepata msaada wa daktari kwa kuangaliwa visababishi na kuvishughulikia.
 
Kwenda hospital kunatofauti

Ukizingatia how sensitive afya ya uzazi is.

Ila kama unaridhika na hapa, well

Hao magyno pia wanaaccount humu ndani thats why nimesema kwa mwenye utaalamu na hilo.
 
Umeshaambiwa kila kitu kina pande mbili,upande wa faida na upande wa hasara! Hizo ni lazima ziwe na madhara tu baadaye sasa iv unaweza usijue lolote! Subiri wenyewe wanakuja kukujibu!
 
Umeshaambiwa kila kitu kina pande mbili,upande wa faida na upande wa hasara! Hizo ni lazima ziwe na madhara tu baadaye sasa iv unaweza usijue lolote! Subiri wenyewe wanakuja kukujibu!
Ndiyo nafahamu hilo,bt hua tunapima,madhara yasizidi faida.
 
Lol hizo pad zikizuia labor pains utakua safi sana
 
mmmh!!! Nina mashaka kama hazitakuwa na madhara maana nina maswali ya kujiuliza, inapunguza utokaji wa damu kwa nini? Zina nini? Pili inapunguza maumivu ya tumbo unataka kuniambia kuwa zimewekwa pain killer???? Mimi naamini Mungu alivyotuumba kwa utaratibu huu alikuwa na makusudi sasa wewe unataka damu ipungue kutoka kwa nini? Pia kwa suala la maumivu ya tumbo ni kawaida na kuda dawa za kutuliza maumivu kwa nini usitumie dawa? Huu ni mtazamo wangu lakini ila TAFAKARI NA CHUKUA HATUA.......
 
si uiache itoke isipotoka ndo inamadhara makubwa,kama unatatizo ya maporomoko yanayozidi kamuone dactari,kwa pads aaaah hapana sitaki kukuamini kirahisi hivi bib NO!huenda uzee unakubimp pia husabisha maporomoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…