Pafyumu: Unajuaje....

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,804
Reaction score
12,227
Kuna siku nilikua pale DSE kumuulizia Broker mmoja (wakiume) nikaambiwa hayupo,,mara mdada mmoja akadakia kwa kusema,,"afadhali leo hakuja kwani pafyume yake huwa inakera.

Leo nimeingia ofisi moja kuna wadada na wanaume wanajadili mdada mmoja ambaye ni secretary,jinsi ya kumwambia, kwani pafyumu yake huwa inawakera pindi anapokatizakatiza kwenye makoridor.

Kama mjuavyo kuna brand tofautitofauti za pafyumu:-

-Sasa wakuu, hiyo pafyumu uliyotumia unajuaje kuwa haiwakeri wenzako?
-Ivi unapaka pafyumu kwasababu unaipenda au wenzako wataifurahia manukato yake?
-Unauhakika gani kuwa hujadiliwi kuhusu pafyumu unayotumia?

Kiukweli mimi huwa situmii kabisa pafyumu wala lotion,na mafuta ninayotumia ni yale yasio na harufu kabisa kama Vaseline na Nivea, yote haya kuepuka kumkwera mtu yeyote.
 
Ila ukweli kuna perfume zinakera. Yaani akipita mtu kwenye corridor yaani unahisi kukereka
Muhimu maeneo kama ofcn au public places mtu lazima aepuke kuwa na perfume au manukato mengine ambayo harufu yake ni kali mno kiasi kwamba wengine inawakera.
Maana kila mmoja akiwa na perfume yenye harufu kali ndani ya ofc hakutakalika
Natumia perfume ila najitahidi sana kutumia zile ambazo hazina harufu kali za kukera
 
Mimi natumia ninayoipenda. Sijawahi ambiwa kama inawakera wenzangu au la....Ikitokea nawakera nitabadilisha.
 
Mimi natumia ninayoipenda. Sijawahi ambiwa kama inawakera wenzangu au la....Ikitokea nawakera nitabadilisha.

Mkuu usitegemee kuambiwa live,,pengine wanakuongelea pembeni. Sasa huoni kuwa unawakera wengine?
 
Mimi minayotumia najadiliwa sana lakini kwa uzuri wake hata bosi aliwahi kunibananisha eti nimtajie jina la pafyumu nayotumia mana anaipenda...lol
 
Ustaarabu ni kupaka perfume ambayo harufu yake itasikika pale mtu atakapokukaribia sana tu na si vinginevyo
 
mie ni mpenzi mkubwa wa perfume....

ila natumia zisizo na harufu kali (perfume kali hunipa mafua,) pia sipeni harufu kali, napendelea harufu iliyotulia, isiyoumiza pua na si yenye harufu kali mpaka ukipita watu wajue Badili tabia kapita hapa.

ila perfume kali huumiza, huleta mafua na sometimes hata kichwa kuuma. ila ndo hivyo kila mtu na mapenzi yake na kila mtu ana uamuzi wa kupaka aina ya perfume aitakayo.
 
Nadhani kutumia pafyumu isiyo na marashi makali na kutpuliza kidogo itasaidia...tatizo kuna watu huwa wanaoga pafyumu....
 

Tatizo wengine wanajipulizia perfume huku hawajaoga sasa mchanganyiko unakuwa balaa....mwingine anajiogesha ile perfume bila kujua mwisho wa siku itaumiza pua za watu huko anaokoenda au wale wadada wakiarabu wanaojifukizia udi kibaaaaaao.....otherwise,mimi nina specific brand ya spray na perfume na ninaamini siumizi pua ya mtu nikipulizia...
 
je?ilee perfume orijinooo ya maraster nayoo ina wakeraa wengine.wathunguu wanaependaaa...ukipanda daladalaaa unanukia arufu ya perfume ya peter toshii watu wote watakutolea macho.hahhaa
 
Mkuu usitegemee kuambiwa live,,pengine wanakuongelea pembeni. Sasa huoni kuwa unawakera wengine?
Nimewahi ambiwa tu kuwa ni nzuri, hiyo ya kuwa inamkera mtu sijaambiwa. Nitabadili endapo nitaambiwa inakera...
 
sasa mnataka simla na yolanda zangu nizitupe?
 
Reactions: TNA

Tuna allergy inayofanana..........naumwa na mafua sana na hataa kuumwa kichwa kama nitakuwa exposed muda mrefu!
 
Sasa kama wenyewe hawamwambii kwamba inawakera atajali vipi hisia zao?

Nwy ni muhimu mtu akajipulizia kidogo tu, ili asisambaze ofisi nzima na kulazimisha hata wale wasiotaka wamnuse.
 
Tatizo watu wengi wanajimwagia perfume badala ya kupiliza kidogo. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu perfume unatakiwa upulizie kidogo, yaani mtu akikusogelea karibu ndio aisikie.

Alafu unapochagua perfume angalia na wheather ya mahali kama inaendana, Mfano sehemu za joto kali kama Dsm unahitaji perfume iliyotulia sio harufu kali. Halafu perfume inapuliziwi kwenye makwapa jamani, maana ikichanganyika na jasho la kwapa 9kwa wenye jasho kali) inakuwa hatari.
 
Ni vizuri kupaka perfume yenye harufu iliyopoa mchana au unapokua ofisini,ili usikere wengine,
kuna watu wana allergy na harufu kali mwisho wanaanza kupiga chafya.

Au unakuta mtu kapaka body spray juu ya nguo kama perfume,kumwambia huwezi inabidi tu unyamaze.

ila ni vizuri unapokuwa na wenzako uwe makini wanaweza wasikwambie kumbe una wakera.
 
raha kamili inakuja pale ambapo mtu kapaka perfume kali halafu haiendani na jasho lake la mwili, utamkimbia....


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…