Paic Kumrithi Maximo Taifa Stars

Paic Kumrithi Maximo Taifa Stars

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,471
Reaction score
752
Kocha+wa+Timu+ya+Soka+ya+Yanga,+Papic+akifafanua+jambo+wakati+Timu+hiyo+ilipoifunga+Simba+Hivi+karibuni+wakati+wa+Kombe+la+Tusker,.JPG

Kocha mkuu aliye matatizoni na uongozi wa Yanga, Kostadian Papic, ndiye atakaechukua mikoba ya Marcio Maximo katika kuinoa Tafa Stars na anatarajiwa kutangazwa na TFF mwezi ujao baada ya kushinda usaili wa nafasi hiyo.

Source: Gazeti la BINGWA la leo.
 
Hayo ni maneno ya wanaomchukia Papic,kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuingilia kesi iliyopo mahakamani.TFF wataona tayari mambo yamevuja hivyo wataamua vinginevyo ,mambo hayo tunayajua sana kwa watz wenye roho ya kwanini wanavyoweza kuharibu mlo wa wenzao.Watz wengi wana roho mbaya sana hata Ben Mkapa alishawahi kuzungumza hilo!
 
Mi ni shabiki namba moja wa S.S.C ila Papic namkubali sana tu, Phiri hakuomba hio kazi ila nae yuko safi.Papic kaibadili yanga kwa 95% nina imani akipewa stars watacheza vizuri sana tena mpira wa kuvutia kuliko hii butua butua ya sasa.
 
Hata akija Morinyo au Capello..tatizo liko palepale....Nchi hii haina mfumo endelevu wa soka....kinachofanyka sasa ni zima moto..hata akija kocha mwenye program endelevu....lazima kuna siasa zitaingia..atakuwa discouraged tu...mwisho wa siku hakuna kitakachoendelea.....ndio maana sifuatilii tena mpira wetu!!!dah!
 
Hata akija Morinyo au Capello..tatizo liko palepale....Nchi hii haina mfumo endelevu wa soka....kinachofanyka sasa ni zima moto..hata akija kocha mwenye program endelevu....lazima kuna siasa zitaingia..atakuwa discouraged tu...mwisho wa siku hakuna kitakachoendelea.....ndio maana sifuatilii tena mpira wetu!!!dah!I love u my country!!
 
Balantanda, Pengo aliposema " kufanya hivyo ni sawa na kuingilia kesi iliyoko mahakamani" nilivyomuelewa hakuwa na maana kuna kesi juu ya Papic au TFF inayoendelea hivi sasa mahakamani! Ila alikuwa na maana ya kuvujisha taarifa kuwa Papic ndie aliyeshinda usaili na hivyo ndio kocha mtarajiwa wa Stars, ni sawa na kuingila kesi mahakamani kwani inaweza kuathiri mchakato mzima na kubadili matokeo!
 
Kilembwe umeongea Kweli. Ila hata mimi ni Mshabiki Wa Mtibwa Suger na Zamani nilikuwa Simba. Ila namkubali Papic Kusema ukweli. Tuache unazi,tuache ushabiki Papic ni kocha Mzuri. Mimi kwa Mtazamo wangu anafaa. Ila wasiwasi wangu siasa za Usimba na Yanga zikiendela na Program Mbovu hata Fanikiwa.
 
Pole wapenzi wa mpira...kama kweli papic atakuwa kocha wa taifa stars basi tusitegemee jipya...utaanza ushabiki wa simba na yanga ktk uteuzi wa timu ya taifa na matokeo yake ni kuwa maximo namba mbili.....
 
Balantanda, Pengo aliposema " kufanya hivyo ni sawa na kuingilia kesi iliyoko mahakamani" nilivyomuelewa hakuwa na maana kuna kesi juu ya Papic au TFF inayoendelea hivi sasa mahakamani! Ila alikuwa na maana ya kuvujisha taarifa kuwa Papic ndie aliyeshinda usaili na hivyo ndio kocha mtarajiwa wa Stars, ni sawa na kuingila kesi mahakamani kwani inaweza kuathiri mchakato mzima na kubadili matokeo!

Nimekusom mkuu..................My bad...........
 
Balantanda, Pengo aliposema " kufanya hivyo ni sawa na kuingilia kesi iliyoko mahakamani" nilivyomuelewa hakuwa na maana kuna kesi juu ya Papic au TFF inayoendelea hivi sasa mahakamani! Ila alikuwa na maana ya kuvujisha taarifa kuwa Papic ndie aliyeshinda usaili na hivyo ndio kocha mtarajiwa wa Stars, ni sawa na kuingila kesi mahakamani kwani inaweza kuathiri mchakato mzima na kubadili matokeo!
Kama tamwacha basi itakuwa ni kwa sababu hawakumtaka lakini siyo sababu eti Kilembwe na Monsignor wamepata habari kabla hazijatoewa na tiefuefu
 
Back
Top Bottom