- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekuwa nikisikia watu wakisema usicheze na paka au usikae naye karibu utapata pumu, je hii ni kweli?
- Tunachokijua
- Paka ni mnyama wa kufugwa anayeishi na binadamu katika makazi yake, watu wamekuwa wakifuga paka kwa malengo tofauti ikiwemo kama urembo huku wengine wakimfuga kwa ajili ya kuwinda panya kwenye makazi yao. Zimekuwepo taarifa kuwa Paka husababisha Pumu kwa watu wanaokaa naye karibu.
Pumu ni ugonjwa unaoathiri mapafu na mfumo wa upumuaji kwa ujumla wake ni hali ya kudumu (inayoendelea), na inahitaji usimamizi unaoendelea wa matibabu. Watu wenye ugonjwa wa pumu wamekuwa wakikabiliwa na dalili mbalimbali ikiwemo kifua kubana au kuwa na maumivu, kukohoa, na changamoto katika upumuaji.
Ukweli upoje kuhusu paka kusababisha Pumu?
JamiiCheck imepitia tafiti na machapisho mbalimbali na kubaini kuwa Paka huchechemua Pumu kwa watu wenye Pumu inayosababishwa na mzio (Allergic Asthma).
Paka wote wanazalisha visababishi mzio (allergens) ‘Protini’ ambavyo vinasababisha Mzio (allergy), hivi vinapatikana kwenye unyoya, mate na ngozi yake. Vigezo vya urefu wa manyoya ya paka, jinsia yake na kipindi anachotumia kukaa ndani havihusiani na kiwango cha visababishi mzio kinachoweza kutolewa.
Visababishi mzio vinavyozalishwa na Paka vinaweza kusababisha ‘allergic reaction’ kwa baadhi ya watu ambapo inaweza kusababibsha dalili za Pumu kama vile changamoto katika upumuaji, na kukohoa.
Pumu ya mzio ama pumu inayosababishwa na mzio (Allergic Asthma or allergy-induced asthma) ni aina ya pumu ambayo viashiria vyake huchochewa baada ya kuvuta hewa yenye visababishi mzio ikiwemo kutoka kwa wanyama wafugwao nyumbani, na vumbi kutoka kwenye mfumo wa uzazi wa mimea.
Aina hii ya Pumu husababisha changamoto katika mfumo wa upumuaji kwa kusababisha njia za hewa kubana unapokuwa unavuta hewa iliyoambatana na visababishi mzio. Unapokuwa na mzio mwili hujilinda dhidi ya hatari yoyote itokanayo na visababishi hivyo. Mfumo wa kinga mwilini hujitahidi kadri uwezavyo kujilinda dhidi ya hatari hiyo, ambapo kemikali mbalimbali huzalishwa zinazoweza kupelekea kuvimba, au uvimbe, na kubana kwa njia hewa wakati huo mwili unapoukuwa unajilinda.
Watu wenye hatari kubwa ya kupata pumu ya mzio ni watu wenye mzio ama kutokea kwenye familia yenye historia ya mzio.
Njia tofautitofauti zinaweza kutumika ili kusaidia kuepuka pumu inayochechemuliwa na Paka, mathalani kumuweka paka mbali na kitanda, chumba cha kulala ama kwenye fenicha.