Paka Oscar aliyekuwa maarufu katika vita ya pili ya dunia

Paka Oscar aliyekuwa maarufu katika vita ya pili ya dunia

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464
IMG-20200507-WA0036.jpg

Kwa mara ya kwanza paka huyu aliyekuwa na rangi nyeusi na nyeupe alikuwa anamilikiwa na mwanajeshi wa Ujerumani Bismarck, na alikuwepo katika safari ya meli ya Ujerumani ya mei 18, 1941 wakati meli hiyo iliposafiri majini kwa siku nyingi kwenda Rheinübung kwa oparesheni maalumu ya kivita.

Kwa bahati mbaya meli hii ilizama mei 27, 1941 baada ya vita kali baharini ambapo ni watu 115 tuu walipona kati ya zaidi ya Watu 2,100 waliokuwa ndani ya meli hiyo, Oscar pia alipona baada ya kuokoloewa masaa mengi baadaye na mwanajeshi wa Uingereza Cossack.

Cossack hakulijua jina la paka huyo, ndipo wakamuita Oscar na rasmi kuwa mali ya jeshi la majini la Uingereza.

Oscar aliendelea kumilikiwa na jeshi la majini la Uingereza kwa miezi kadhaa huku akisafiri nao mara kwa mara kupitia usafiri wa maji hadi Oktoba 24, 1941 ambapo meli yao ilipotoka Gibraltar kwenda Uingereza, na siku 3 mbele wakiwa safarini ikashambuliwa na kuzama.

Zaidi wa wanajeshi 1,000 walifariki, waliopona walikuwa 159 pekee akiwemo Oscar ambaye baadaye alipelekwa katika kambi ya jeshi la Uingereza huko Gibraltar.

Oscar sasa akapewa jina la Unsinkable Sam, yaani asiyezama. Akachukuliwa na kikosi cha majini cha Ark Royal cha UK ambako huko nako ilishambuliwa na kuzama November 14, 1941. Haijulikani meli hii ilibeba wanajeshi wangapi, lakini safari hii ni mwanajeshi mmoja tuu alipona, Oscar pia alipona.

Baada ya kuokoloewa akarudishwa Belfast UK alikoishi hadi anafariki mwaka 1955.

Written by MILITARY Genius

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...
Baada ya kuokoloewa akarudishwa Belfast UK alikoishi hadi anafariki mwaka 1955.
... "fariki" is a reserved word for human beings only. Wanyama including huyo paka wanakufa na sio kufariki. Another word in honor of human beings is "jifungua" instead of "zaa".
 
Cats are arrogant creatures.Ila napenda sana kampani yao.Anajua anatakiwa ajisubmit kwa binadamu lakini kiburi tu.
 
Back
Top Bottom