Paka wenye tabia hizi huwa ni paka kweli?

Paka wenye tabia hizi huwa ni paka kweli?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Anapenda kwenda sawa na wewe kwa kile unachokila na muda mwingine atataka ale zaidi yako.

2. Ukiwa umelala na mkeo au mpenzi wako atalazimisha akupige chabo dirishani.

3. Ukiificha mboga hasa nyama sehemu ya mbali akiwa hayupo baadae unakuta ameshaila.

4. Ukimuadhibu anakudindia (anakukazia) na muda mwingine anaweza hata Kukutoa baru (Kukukimbiza)

5. Hata kama akiwa mbali vipi lakini Ratiba zote za Wewe Kula anazijua na hachelewi hata Sekunde.

6. Ukiweka wimbo wa UNO wa Harmonize utamuona nae anaufurahia huku anatikisa mkia wake.

7. Akikuona unautizama wimbo wa Baba Lao wa Diamond runingani anaenda kuzima swichi kabisa.

Wenye paka, tafadhali naomba uzoefu wenu nanyi ili nijue ni paka wangu tu au hata na wenu pia.
 
Huyo ni paka mtu

Naanza Kukubaliana nawe Mkuu kuwa yawezekana nikawa naishi na Binadamu Mwenzangu ila sema Mimi tu sijui. Na Kinachonishangaza zaidi ni kwamba kwa Kupatwa nae na Hasira nimeshawahi Kufanya jaribio lisilotakiwa na Watu wa Maliasili na Haki za Wanyama la Kumuwekea ' Sumu ' ili apotee kabisa lakini mara zote nikifanya hivyo huwa anakuwa hayupo kabisa na zile Siku ambazo huwa nakuwa sina nia hiyo ndiyo huwa nashinda nae Kutwa tena huku akijiachia kabisa.
 
No 7 hapo muulize kwanini hampendi mondi kama hana majibu ya kueleweka mfukuze kwako
 
Rais mwenye tabia hizi huwa ni rais kweli?

1.Anapenda kujimwambafy
2.Hataki kusikia neno upinzani
3.Anawaza kutawala hadi afe
4.Anataka chartlle iendelee kuliko dodoma
5.Kinara wa kuteka wapinzani
6.Ufisadi wa 1.5 trillion anapotezea anaona ni ufisadi kidogo
7.Anavaa nguo za kijeshi kujimwambafy
8.Anapenda asifiwe na bunge
9.Mihimili yote anaweka mfukoni
10.Nchi wahisani wake ni Zimbambwe
11.Wanaomchangia budget kwa asilimia 60 anawaita ni mabepari
 
Naanza Kukubaliana nawe Mkuu kuwa yawezekana nikawa naishi na Binadamu Mwenzangu ila sema Mimi tu sijui. Na Kinachonishangaza zaidi ni kwamba kwa Kupatwa nae na Hasira nimeshawahi Kufanya jaribio lisilotakiwa na Watu wa Maliasili na Haki za Wanyama la Kumuwekea ' Sumu ' ili apotee kabisa lakini mara zote nikifanya hivyo huwa anakuwa hayupo kabisa na zile Siku ambazo huwa nakuwa sina nia hiyo ndiyo huwa nashinda nae Kutwa tena huku akijiachia kabisa.
Acha sasa hizo tabia za kipakapaka
 
Back
Top Bottom