Dogo, leo umeendelea vizuri na dose ya dawa ulizopewa Hospitali Ya Milembe. Keep it up, akili zitakaa sawa tu mdogo mdogo.
Na hata kwa wale wana CCM wenzio waliokua hawaelewei ile kauli ya Mama "ALIESIMAMA HAPA NI RAIS", somo ni gumu kidogo ila taratibu wataelewa tu, kama TPA leo walivyoeleweshwa wakaelewa.
Somo linaendelea muda si mrefu, subiri majibu yaletwe kuhusu amri aliopewa CAG kufanya ukaguzi wa hela zote zilizotoka Hazina kuanzia January 2021 - Mpaka mwezi huu. Hapa waliochota hela kwa advantage ya Rais kuumwa na kwa kisingizio cha matumizi ya msiba wa Rais - Wataelewa somo vizuri pia (Iwe kuna Waziri, Naibu Waziri, Katibu, Muweka Hazina au yoyote kama amehusika, basi ataelewa somo).
Mama amecheza karata zake vizuri sana, kama ikitokea kuna Mawaziri au Manaibu Waziri (Hasa waliokua hawamtii kipindi yeye ni Makamo Wa Rais, na waliokua wakidiriki hata kumchongea kwa Rais pindi alipokua akiwahoji na kuwauliza baadhi ya maamuzi wanayofanya) wamehusika kuchota hela katika kipindi hicho cha kuanzia January, basi Mama hatawafumbia macho na anapata sababu ya kulivunja Baraza La Mawaziri For Good.
#Mlimpeleka Askofu Gwajima bungeni mkategemea aende kuichambua "REPORT YA CAG" kweli. Wakati report ya michango ya kanisa lake hajui kuichambua kwa waumini wake.