Pamba Jiji wavunja Mkataba na Kocha wao Goran Kopunovic

Pamba Jiji wavunja Mkataba na Kocha wao Goran Kopunovic

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Sema tayari kimeumana! Hawa Pamba Jiji Championship inawaita mzunguko wa kwanza tu 😃​
1729093693852.jpg

Uongozi wa Klabu ya Pamba Jiji Fc unautaarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Goran Kopunovic.

Lakini pia umefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya wasaidizi wake, Salvatory Edward, Kocha wa magolikipa Razack Siwa na kocha Viungo Cirus Kakooza.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mathias Wandida aliyekuwa kocha wetu wa U-20 hadi hapo atakapotangazwa kocha Mkuu.

Uongozi unawashukuru kwa muda wao wote waliokuwepo hapa klabuni na unawatakia kila la kheri katika maisha yao nje ya Pamba Jiji.

Imetolewa na:
Ezekiel Ntibikeha,
Kaimu C.E.Ο,
16 Oktoba, 2024
 
Mechi ya mwisho ya kupanda daraja walipewa matuta mawili hapo Arusha nikasema hawa nguvu ya mpira hawana huko juu nguvu ya kuwanunua marefa kama huku chini hawana watapotea sana..
Kasi ya NBC ni kubwa Pamba hawezi kumudu! Huku ni zaidi ya dakika 90 za uwanjani 😃
 
Mathias Wandiba dogo wa Ilala,Iringa,nimecheza nae sana chandimu Iringa,alikuwa Geita akimsaidia Minziro kwa muda mrefu,nadhani anaweza kuisaidia Pamba akipewa support
Tokea alivyoondoka Makalla sijui Pamba Jiji imekuwaje tu!??
 

Amos Makalla umeondoka na Pamba Jiji 😔
 
Mzungu wa watu wamemvunjia mkataba mapema
Huyo mzungu amewahi kufanya maajabu kwenye team gani hapa Tz? Alikaribia kuishusha daraja Tabora Utd, kama si uongozi kufanya maamuzi magumu ya kumtimua dakika za lala salama Tabora ingekua championship muda huu. Kutimuliwa Pamba lilikuwa suala la muda tu kutokana na mwenendo wa team. Huyo na Mwinyi Zahera ni mapacha.
 
Back
Top Bottom