John Pambalu ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (
BAVICHA) aliyechaguliwa mwaka2019 anayemaliza muda wake kutokana na uchaguzi uliofanyika Januari 13, 2025 huku matokeo yakisubiriwa kwa hamu ili kupata safu mpya ya uongozi wa baraza hilo.
Kabla ya tukio la upigaji wa kura kufanyika ulifanyika
mkutano katika ukumbi wa Ubungo Plaza ukihusisha wajumbe wa Baraza hilo huku viongozi wakuu wa chama hicho wakihudhuria akiwemo mwenyikti wa
CHADEMA Freeman Mbowe na makamu mwenyekiti Tundu Lissu ambo wote walipata nafasi ya kuhutubia mkutano huo. Kadhalika mwenyekiti wa Baraza la Vijana anayetamatisha muda wake wa uongozi alihutubia mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine Pambalu
alikemea kuhusishwa kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.
Kumekuwapo
kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kinachomuonesha Pambalu akisema ‘’ukiwa na laki tatu tukawakamata wajumbe, tukawalaza wajumbe watakuchagua kuwa mwenyekiti wa Bavicha’’
Je ni upi uhalisia wa kipande hicho cha video?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutokana na kukatwa kutoka sehemu ya hotuba ya John Pambalu kwenye mkutano mkuu wa BAVICHA, hivyo kuondoa baadhi ya maneno yanakamilisha ujumbe halisi uliokusudiwa na Pambalu. Tazama
video halisi hapa kuanzia dakika ya 6 sekunde ya 38.
View: https://youtu.be/EO26-rU_QDI?si=qaa_CMnl-vvWiEBn
Katika hotuba yake inayohusisha sehemu hiyo ya video mwenyekiti huyo wa BAVICHA alikuwa akisimulia pindi alipokuwa mdogo ambapo mama yake alikuwa ni sehemu ya uongozi wa CCM UWT ngazi ya kata, jambo lilopelekea baadhi ya vikao kufanyika nyumbani kwao na hivyo kumfanya atake kujua ni namna gani anaweza mwenyekiti wa UVCCM katika kata Butimba ambapo aliambiwa atafute shilingi laki tatu.
“Mama yangu alikuwa katibu UWT kata, vikao vya CCM vilikalia nyumbani nikiwa kidato cha tatu, mimi nikawauliza nifanye nini niwe mwenyekiti UVCCM Kwenye kata yetu ya Butimba? wakaniambia ukiwa na laki tatu tukawakamata wajumbe, tukawalaza wajumbe watakuchagua kuwa mwenyekiti wa UVCCM. Wakaniambia mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye ndoto ya kuwa kiongozi anawauliza nikitaka kuwa kiongozi kwenye chama chenu nifanye nini wakaniambia tafuta laki tatu, wachukue wajumbe, walaze wajumbe, tulivyomaliza ibaada ya jioni nyumbani nikawaambia wazazi wangu chama chenu sitojiunga nacho kwa sababu hawamchangui mtu kwa uwezo wake bali kwa sababu ya pesa”
Hivyo kipande hicho cha video kinachosambaa mtandaoni kina nia ovu ya kusambaza ujumbe usiofaa kutokana na kutokukamilika kwa kipande hicho.
Tazama
hapa hotuba nzima ya John Pambalu katika mkutano huo.