Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Pambano la jana kati ya Mwakinyo na mfilipino baada ya kuisha. Watanzania wengi tumejitahidi kuelezea hisia zetu juu ya hili pambano. Na nimesikitika kuona watanzania wengi wanalalamika kuwa Mwakinyo kabebwa.
Hili pambano limepelekea nirudishe miaka nyuma kidogo, nakumbuka kipindi kile tukiwa wadogo ilikuwa ukiangalia ngumi za kwenye video unaamini kabisa na wewe una nguvu kama za Schwarzenegger au Vandamme na wakina Blucelee kupitia kuona. Na baadhi yetu kuna watu tuliwaogopa tukiamini anapiga kama za kwenye video.
Leo hii naona watu wanaleta hadithi za kitoto kuwa jamaa hawezi kwa kuona tu kwa video. Mchezo wa ngumi ni tofauti na michezo mingine. Hawaangalii umepiga ngumi ngapi bali zinahesabika ngumi ambazo zimemfikia muhusika mahala husika. Mwakinyo kwangu ni mastermind alimsoma mpinzani wake akajua huyu ni butuabutua. Muda mwingi Mwakinyo alimsoma mpinzani na alihakikisha anapiga ngumi za point tu.
Na yule jamaa aliyepigana naye siyo mnyonge ndio maana waliweza kumaliza round zote.
Sisi wenyewe tunapenda kukatishana tamaa wenyewe na ujuaji ndio unaotuponza wa kila kitu. Sasahivi kila mtu ni mtaalamu wa ngumi. Mwakinyo kafanya vizuri sana nadhani ndio huu mwanzo wa kuamini wakina Mwakinyo wengi ili waweze kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Wito wangu kwa mapromota wa ngumi na wapenzi wa hizi ndondi tukishirikiana na serikali yetu huu mwamko mlionzisha juu ya ndondi uendelee hivihivi na hii itasaidia sana hata wapiga ngumi wengi iwe sehemu ya kipato chao.
Najua mitaa yetu imejaa vipaji vya wapiga ngumi ila asilimia kubwa ya hao wanatumia vipaji vyao katika mambo ya kiuhalifu kama wizi na uonevu ndani ya jamii zetu.
Mlimwengu mimi nimefurahia sana mapambano ya jana kuanzia kwenye mechi za ufunguzi mpaka mechi yenyewe. Vipaji vipo na nia ipo hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha tunasaidia sekta hii ya ndondi inapata heshima yake na kuweza kufika mbali katika level za kimataifa.
Tusichukulie poa yule Mfilipino anagonga balaa. Ukiwa mdebwedo dakika sifuri tu unatapika mchuzi.
#mlimwengumimi
#champMwakinyo
#ndondindodini