Niliishawahi kusema hapa kuwa kuna haina tatu za watu ndani ya CCM
1. Wenye dhamira hai
2. Wenye dhamira zinazoelekea kufa
3. Wenye dhamira mfu
Wachache wamefikia kwenye dhamira mfu na hao ndo unawaona kwenye vyombo vya habari wakiishabikia CCM eti imeshinda huku wakijua si kweli lakini kwa kuwa dhamira zao ni mfu hawaoni haya.
Kwa kuwa wengi wa CCM wako kwenye kundi la 1 na 2 na wanajua nini kimefanyika mpaka wanajiita washindi, naomba uudhurie mojawapo ya sherehe zao za ushindi utangundua kuwa wengi roho zao zinasononeka maana hawasherekei ushindi wa kweli, ni suhindi wa hira na dhamira zao zinawasuta!
Anayeiba hawezi sahau aliyemwibia hata siku moja!
Naomba siku moja mnipe mwonekano wa watu wa ssm katika sherehe zao na hasa subiri siku ya kuapishwa rahisi utaona atakavyokuwa akiongea, uso wake utakuwa kioo cha madhambi aliyoyatenda!