Uchaguzi 2020 Pamoja na kuzima internet kuna watu wanaumia kimoyomoyo, ila wanashangalia na kupongeza "Chuma kimechukua nchi"

Uchaguzi 2020 Pamoja na kuzima internet kuna watu wanaumia kimoyomoyo, ila wanashangalia na kupongeza "Chuma kimechukua nchi"

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Watanzania tusingekuwa wanafiki, basi wote tungepaza sauti kupinga kitendo kilichofanywa na Serikali kwa kutoa amri ya kulimit internet access, lakini kwa sababu ya hofu, watu wengi wanaumia moyoni huku wakiamua kushangalia na kupongeza ushindi wa kishindo kwa Chama cha Mapinduzi.

Lakini tuseme ukweli kila mtu ameathirika na kitendo hiki na ukizingatia kuwa hakukuwa na sababu ya kuzuia internet, badala yake walitakiwa kuandaa mazingira ya uchaguzi huru na haki ambao ungewaacha watu wote wakiwa wameridhika na kila aina ya matokeo.

CCM walijua kuwa uchaguzi hautakuwa Huru na Haki hivyo kuna kila dalili za watu kuyakataa matokeo hivyo.
 
Chuma bana anavaa mashati ya gharama na ghali wakati uchumi wa nchi hupo ICU. Kama kiongozi a natakiwa awe Mfano katika kipindi hiki kigumu watanzania tunapitia.

a6e8e7ad7c3609cd13a1e4e4effb1301.jpg
 
Mimi Nadhani wangetuarifu tuu kwamba internet itafungwa ,hawajatumia busara Kama walipata hofu yakuingiliwa na mataifa ya nje ni vyema tuu wakaanzisha mitandao ya ndani ya nchi ambayo hayataingiliwa na nchi nyingine
 
Kila matokeo ya uchaguzi iwe somo, Chadema inatakiwa itengeneze na kuimarisha Party Organisation ili kupambana na political contest yeyote. Wakati uchaguzi ukifanyika mimi nilikuwa Jimbo la Hai na hasa hasa Lyamungo Sinde..

Kama jimbo la Mwenyekiti tuu Party Agents katika vituo vingi walikuwa wa kujitolea na hawaaniki, sijui maeneo mengine inakuwaje. Tutapigwa sana lazima tujipange sawa sawa.
 
Ushindi wa Kishindo...Unashindana na Mpizani wako huku umemfunga miguu na Mikono. Unaamua Kumpa Mpinzani wako Kura Kiduchu ili kujustifahi asivyopendwa. Waacheni Walioshindwa Wawe huru hili wafanye tathimini ya wapi walifail miserably...Kwa ajiri ya maandalizi ya 2025, AU ndio basi hadi uchaguzi 2025.
 
CCM walijua kuwa uchaguzi hautakuwa Huru na Haki hivyo kuna kila dalili za watu kuyakataa matokeo
Hii pamoja na kuzuia maandamano ndizo sabb za kuzima mitandao, ili wengi wasijue kinachoendelea.

Pia kwa baadhi ya maeneo huko mikoani na vijijini, Kuna kamata kamata hatari inaendelea ili kuzima uasi, nk.

Redio Kama BBC, VOA, DW.. nk ni vigumu kupatikana, hasa wakianza kuongelea uchaguzi wa Tanzania. Redio za ndani zishapigwa pini kitambo
 
Back
Top Bottom