Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,506
BOBI WINE anasema alikataa kuonana na Rais Museveni alipokwenda kumtembelea kwa siri Gerezani. Bobi akagoma kuondoka mahakamani hapo alipoletewa ambulance hadi wenzake 33 watakapokamilisha dhamana zao. Jaji alianza na Bobi ili kupunguza 'JAM' mahakamani.
TUJIFUNZE masuala kadhaa kutoka kwa huyu mtu. Sio kosa pia. Kuna kitu ndani yake. Anaweza asiwe amepita kwenye mengi lakini ameonesha 'uthabiti' na 'uimara' wake kwa ambayo ameamua kusimamia. Anapigania anachoamini ni sahihi. Anaitwa "President of the ghetto"
Jaji amesema Bobi Wine atibiwe popote hata nje ya nchi ikiwezekana. Amekata OMBI la upande wa jamhuri lilikuwa likimtaka Bobi akabidhi passport yake ya kusafiria. Ameitaka serikali irejeshe passport yake mikononi kwa Bobi wine. Kwa sababu ni mbunge ana haki hizo.
Pamoja na hali ngumu ya kisiasa nchini Uganda, bado Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha DP, Norbert Mao ametangaza rasmi kwamba kuanzia kesho 28.08.2018 saa tisa jioni saa za Afrika Mashariki 'umoja wa upinzani nchini Uganda' unatangaza operation inaitwa "MUSEVENI MUST GO"
DR. Warren Kiiza Besigye Kifefe 'The Hammer' alikuwa mahakamani hapo, akatoa huduma ya kwanza kwa mtuhumiwa mmoja aliyeanguka na kuzimia, ni daktari, amewahi kuwa daktari wa MU7, anasema nchi haiwezi kusubiri uchaguzi 2021 Museveni akiwa Rais, wakati wananchi wanauwawa na kuuwawa.
Pamoja na mengi yaliyotokea katika sakata hili la Kyagulanyi Robert Ssentamu (Bobi wine), kinyume na haki zake za binadamu; mbunge wa Kyaddondo East dhidi ya serikali ya Museveni; nimejifunza masuala kadhaa kuhusu Uganda;
1. Uhuru wa mahakama
2. Uhuru tume ya uchaguzi
3. Uhuru wa mijadala
4. Uhuru wa bunge
#MMM
Sent using Jamii Forums mobile app