johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Baniani mbaya kiatu chake kizuri na usione vyaelea vimeundwa.
Unapoona mtu anatoka kwenye chama kidogo kama Chadema na kwenda chama dola na moja kwa moja anapata uteuzi wa Rais basi elewa chama alichotoka kimemjenga akajengeka.
Binafsi huwa simfagilii Mbowe lakini kitu kimoja huwa nakikubali Freeman Mbowe anajua kuwasuka vijana.
Waangalie Juliana Shonza, Katambi na Mwita Waitara aliyekuwa muhudumu wa Dkt. Nchimbi pale UVCCM wote wamepita katika mikono ya Freeman na sasa ni viongozi wa kutegemewa chama tawala.
Hata huyu Halima na Mnyika ni Freeman kawatengeza. Nakumbuka Mnyika wakati anaanza siasa alidakwa na mzee Malecela lakini sikumbuki aliponyokaje tukasikia Mbowe kamsajili Ufipa.
Anyway mambo ni mengi muda mchache lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Huwezi kukijua kitu bandia kama hujawahi kukiona halisi.
Maendeleo hayana vyama!