Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 911
- 3,017
Uchawi wa mpira now days upo kwenye nguvu ya viungo katikati ya uwanja.
Zamani uchawi wa mpira ulikuwa unaamuliwa na kasi ya mawinga ndio maana mawinga kama akina Ribbery, Arjen Robben, Wright Phillips, Theo Walcott na wengine wengi walitisha sana kwa kasi zao.
Lakini mifumo ya mpira ulipobadilika kazi ya mawinga kuwa na mbio kwa kutanua pembeni sio issue sana ndio maana unakuta winga mashoto badala ya kucheza no. 11 anachezeshwa winga no. 7 ili kwa kasi yake na guu la kushoto afosi kuingia katikati ya uwanja. Sasa mawinga wanapo fosi kuingia katikati means wanataka kuongeza namba ya viungo katikati.
Turudi kwa timu ya Simba, Simba inazidi kuimarika sana kila idara jambo ambapo ni zuri sana lwa timu inayopambania ubingwa wa nchi.
Kama tulivyosema, mpira wa kileo unaamliwa sana na viungo wa katikati (viungo wakabaji na viungo washambuliaji).
Kwenye viungo washambuliaji, Simba haina shida sana kwa sababu ina namba ya kutosha. Changamoto ipo kwa viungo wakabaji: partnership ya YUSUF KAGOMA na FABRICE NGOMA ni babkubwa. Fabrice Ngoma amepunguza sana yale makosa yake ya kuchelewesha mpira kwa kupiga chenga za kuzunguka na kurudisha mipira nyuma kwa mabeki mara kwa mara. Hapo hongera sana kwa Fabrice Ngoma.
Kiungo Yusuf Kagoma, huyo bwana mdogo ni habari nyingine kabisa. Anafika miguuni kwa adui kwa haraka sana na kuchukua mpira. Anainua kichwa kuona mpira aupige kuelekea wapi jambo ambalo huwezi kulipata kwa kiungo Mzamiru Yassin.
Hivyo ili Simba iendelee kuwa mbele ya kila mpinzani anayecheza nae, nashauri viungo wakabaji no. 6 waongezwe kwenye timu ili tuwe na uhakika wa ukabaji hasa unapokutana na mpinzani ambaye anashambulia sana.
Hivyo kwa kuzingatia hilo usajili wa wachezaji hawa mmoja wao kwa nafasi ya kiungo Mkabaji utatufaa sana. Hawa ni viungo wa shoka kweli kweli utopolo wanajua kazi yao. Kiungo wa kwanza ambaye inabidi aje msimbizi ni ADOLPH MTESINGWA BITEGEKO wa Azam FC hanaga kucheka na kima huyo.
Wa pili ni ANDY BIKOKO kutoka Tabora United huyu alizima viungo wote wa utopolo wakala chuma 3 kama wamesimama.
Toa kwa mkopo wachezaji hawa Mzamiru Yassin, Kalabaka, Okajepa, Joshua Mutale, ili uwapate wachezaji hao Andy Bikoko au Bitegeko.