Pana upendo hapa au ndo kuwa mshika pembe?


she loves u now cos ure in states that is all about!
 
Atakaa mambo makubwa if that is the case ATAMEGWA endlessly coz mambo makubwa hayaishi daily yanaibuka makubwa zaidi ya jana! Bora aendelee kumegwa akiwa nje ya Himaya yako!
 
Bado 2 hujamremove kwny fb friends? Akili kumkichwa kakayangu its so obvious amedatishwa na kuwa kwako US.. Cjui wanawake wengine 2nakuwaga na akili gani aaagh!
 
wanabadilika zaid ya kinyonga,
Anyways, najua binadamu, wake kwa waume, wanapenda kuwa karibu na watu wenye mafanikio, fair enough..lakini huyu mdada ameniacha kinywa wazi kwa kweli, na hana hata mshipa wa ayb, maana mwanzo alimwambia msela asimtafute yuko bize na brazamani mpya..sasa kapiga U-turn kali sana na anasema mapenzi ya mbali anayaweza na anampenda sana jamaa..lolz..this is hilarious.
 
Kaka huyo maneno aliyokwambia siku za nyuma kuwa hawezi kumkwaza Mpenzi wake na yale ya kuwa hawezi kuwa na mpenzi wa mbali lakini kumbuka mlikuwa Tanzania kipindi hicho leo anaona upo USA basi anaona ataweza kuwa na mapenzi ya dhati kama hutaki kujitia achana nae kwani atakutesa sana.Kingine anaoneakana hana msimamo hivyo hata ukiwa USA utaendelea kumegewa tu.

Mimi sikushauri kamwe kujiingiza kwenye mahusiano na huyo mdada atakuumiza sana .Anaonekana anapenda maisha fulani ya mapenzi ya muda mfupi.
 

Hakufai kua mke wako.
Mweleze ukweli huna mpango nae katika kua mkeo.
Ila muulize matatizo yake alio nayo...kama bado wampenda umsaidie hizo shida zake.
Ndio anastahiki.
 
naona wengi hapa wana mwona mwanamke kama mtu wa kudandia mafanikio ya mwanaume kwa ulaghai wa mapenzi. maisha yana ups and downs na kuna tofauti ya namna ya kubehave ukiwa na mpenzi mpya kwa mwanaume na mwanamke. hii inatokana na utamaduni wetu unaomwona mwanamke kuwa ni wa kumilikiwa na hili limechangia sexual lifestyle ya wanawake kuwa controlled na mwanaume. sasa alipokuzuia usiwasiliane naye kwa sababu ana mtu mwingine ni katika ku-avoid matatizo zaidi kwa upande wake kutoka kwako na kwa huyo mtu wake mpya. kwa kuwa nawe umekiri kuwa ulipata wako mpya, hapo sioni makosa kwake. pia sioni kuwa kwa ilo pekee hata na kwa kukuzuia usiwasiliane naye basi alikoma kukupenda kwa dhati.

imagine yeye angekuwa na kazi nzuri na akasikia umefukuzwa kazi na uko kijijini kwenu huna hata nauli ya kukuleta mjini kutafuta kazi ndiyo akakkuambia kuwa bado anakupenda na yuko tayari kumuacha aliyenaye na kuambatana na wewe licha ya hali yako hiyo ya sasa, ungereact namna gani? je na hapo ungekuwa na shaka na upendo wake kwako? nionavyo mimi, hata wewe pia unababaika na kuwa huko state (kama unavyokuita)! inaonekana kuwa kwa sababu uko state, hata mie judith hapa nikikuambia kuwa nakupenda utaona ni kwa sababu nababaika na state kumbe naweza kuwa kweli nimezama kwenye mapenzi mazito ya kweli na yenye baraka za Mungu. nakuomba sana usiufunge mlango wa mapenzi bali uache wazi ili Mungu mwenyewe awaunganishe, usije ukamkosa mke mwema kutoka kwa Mungu kwa bvile tu uko huko state, kumbuka kwa Mungu hakuna tofauti ya huko state na huku maneromango, bali kote ni sawa machoni mwake
 
Kwenye maandishi hayo mekundu ni nadra sana kukuta mdada ambaye anakazi nzuri kupenda mlala hoi ,Wadada waliowengi siku hizi wanapenda maisha mazuri na wanapenda hata Mume au mpenzi wake awe na maisha mazuri la sivyo ukikuta anapendwa mlala hoi ujue yeye ni mbadala tu ila mwenye nyumba yupo.
Japo uwezekano wa watu wa namna hiyo wapo wengi ila si kwa huyo aliyesema hawezi kuwa na Mpenzi wa mbali wakati wakiwa chuoni.
 
Chukua hatua, kwa wasichana wa sasa ndio tatizo lao . Hawana mapenzi ya kweli wao ni pesa mbele sio mapenzi mbelee. Je kama alisema mapenzi ya mbali hayawezi iringa-dar ,je dar -usa ndo ataweza huyo?
Achanaa naye huyo kimeo hichoo ohhh tafuta wenye penzi la zati huyo hakuna kitu ni linungayembee tu hilo.
 

haaaaaaaaaaaa hakuna kitu kwa wakati huu eti mwanamke mwenye fedha zake ampende mlalalaho e? Na akubali waoane? Labda hilo ni shugamama . Lakini wengi fedha mbeleee, na pia ukiona hivyo ujue kuna mwenye anagonga wewe utakuwa kama mnala tu humo ndani lengo kutoa aibu kuwa na kaolewa kwa ndoa ya msikitini au kanisani.
 
Kama kwa sasa uko na mwingingine na unampenda kwa dhat sioni sabab ya kukushaur umwache uliyenaye sasa then urud kwa mwingine.
 
Huo ndio ukweli wa mapenzi ya siku hizi huna kitu hakuna atakaye kupenda na kukudhamini kuna misemo yao wanasema kuwa hapendwi mtu linapendwa pochi tu so likisha na penzi linaisha
 
kwel ulikaa nje ya jf kuisoma kwanza_umenichekesha pale uliposema et jamaa angekuwa busha hana nauli ya kurudi town na demu akamwambia anampenda ingekuwaje_sasa naamin wanawake mkewezeshwa mtatutupindua_dawa ni mfumo dume
 
 
kuna mapenz ya Bluetooth siku hiz, wakat mkisoma hayakuwepo ndo mana alishindwa kuvumilia_lkn sasa hata uwe wapi mnatumia Bluetooth halafu wenzako wa karibu Wana_socket moja kwa moja kwenye source ivo mnaweza kuhudumiwa weng kwa wakat mmoja
 
Mshirikishe na Mungu pia, maana huwezi kujua yawezekana huyo ndo ubavu wako. Katika safari yoyote kuna kuanguka, kuumia, kukata tamaa lakini cha Mungu huwa kinasimama na kudumu.
:bump:hakuna kitu kama hicho wewe hebu acha kumshauri mwenzio pumba...............hcho ni kimeo tu hbu potezea.NAKABIDHI
 


wanawake wamekuwa hivyo kwa sababu ya imani iliyomo katika jamii kuwa wanasaka mafanikio ya wanaume. na pia wengine wameweka pesa mbele kwa kuwa hana assurance na heshima yake kwenye jamii, hivyo anaona bora afaidi hela tu kama zipo. lakini mie naamini wanawake wenye kupenda kwa dhati na kiukweli wapo tena wengi tu, na Mungu hawezi kushindwa kutubakishia masazo katika nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…