Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
KAGERA SUGAR KUMALIZA NAFASI YA TATU 2017, MSTARI WA KUSHUKA DARAJA SASA NA ANGUKO LA MISIMU SITA NYUMA
KAGERA SUGAR FOOTBALL CLUB kuanzia msimu wa mwaka 2018/19 hadi sasa wanashuka, hapa nitakupa Tathmini yao ya MISIMU SITA kuanzia alama zao kisha idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa pamoja na nafasi walizomaliza, utaelewa taratibu nafasi yao na namna Timu inashuka chini kwenye maeneo tofauti tofauti
Msimu wa 2018/19 wakati ambao Ligi Kuu ya Tanzania ilikuwa na ushiriki wa Timu 20, walimaliza nafasi ya 18 wakiwa na alama 44 wakifunga magoli 33 na kufungwa 43 mbele ya Stand United na African Lyon walioshuka daraja, baada ya msimu huo 2019/2020 Kagera Sugar walimaliza nafasi ya nane wakati huo wakipanda alama zao zikifika 52 wakifunga magoli 44 na kuruhusu 41
Kagera Sugar hapo walisogea lakini bado 2020/21 walikusanya alama 40 katika nafasi ya 12 wakifunga magoli 34 na kufungwa 38 wakati huo Timu zimepungua Ligi Kuu zipo 18, kisha msimu uliofuata wa 2021/22 wakati Timu zikipungua na kuwa 16 wakamaliza nafasi ya sita na alama zao 39 wakifunga magoli 20 na kufungwa 25, huo ni msimu ambao Biashara United na Mbeya kwanza walishuka daraja
Msimu wa 2022/23 walimaliza nafasi ya 11 wakifunga magoli 23 na kufungwa 36 wakati ambao wamekusanya alama 35 pekee, wakati huo Polisi Tanzania na Ruvu Shooting walishuka jumla achilia mbali Mbeya City ambao walicheza playoff na kushuka pia! Hapa ukifanya Tathmini ya misimu yote hiyo utagundua timu inapanda na kushuka katika nafasi zao, idadi ya magoli ya kufunga au kufungwa pia
Kagera Sugar simu uliopita hawakumaliza katika nafasi nzuri sababu walimaliza nafasi ya 10 alama zao zikiwa 34 magoli ya kufunga 23 na 32 ya kufungwa! Timu kila msimu inakuwa na eneo ambalo haiko imara sana, hakuna muendelezo maalumu walionao uwanjani na usajili wao kwa sasa haulipi sana
Msimu huu hawana namba nzuri sana na chini ya Melis Medo kwa sasa wapo nafasi ya 15, alama 12, wamefunga magoli 13 na kuruhusu 27 katika wakati ambao Dirisha Dogo wametumia kusajili viungo watatu na golikipa mmoja pekee! Kagera Sugar haitishi tena kama miaka 10 nyuma na watu hata kuchukua Alama pale Kaitaba Stadium ni kawaida tu.
@Oscarevodius
Let's Goo!!.