Pandu Kificho, ana mamlaka ya kuunda kamati kufuatilia swala la nyongeza ya posho?

Pandu Kificho, ana mamlaka ya kuunda kamati kufuatilia swala la nyongeza ya posho?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi Kificho,kama mwenyekiti wa muda, ana mamlaka ya kuunda kamati ndogo kufuatilia swala la nyongeza ya posho kwa wajumbe wa bunge la katiba?Yeye kama mwenyekiti wa muda si anatakiwa kusimamia uundwaji wa kanuni na sheria za bunge hilo tu?

Hii kasoro hata kama wajumbe wenzake wameiona, wanaweza kujifanya vipofu kwani hata wao watakuwa ni wanufaika wa mapendekezo ya kamati hiyo endapo serikali itayaafiki.

Naomba wanasheria mtujuze uhalali wa jambo hili.

Nahisi Kificho amejipa madaraka yasiyo yake.
 
Wanataka tu kuhalalisha. .. watu wanapounda tume za kujipangia maslahi ni uwehu... watumishi chungu nzima wana malalamiko yao juu ya stahili zao, hawajawahi kuambiwa waunde tume kuchunguza madai yao...
 
Hili swala liko kisheria zaidi ngoja wale wanaojua sheria waje watusaidie mkanganyiko huu..
 
Hapa kitakachotokea ni wajumbe wote kulipwa 420,000 kama hao wa Zanzibar.Tatizo hapa raisi ni mtu dhaifu na pia anategemea bunge hilo lipitishe rasimu itakayomlinda hata yeye atakapoostafu.
 
Hapa kitakachotokea ni wajumbe wote kulipwa 420,000 kama hao wa Zanzibar.Tatizo hapa raisi ni mtu dhaifu na pia anategemea bunge hilo lipitishe rasimu itakayomlinda hata yeye atakapoostafu.
Tatizo lako we mburula hapa rais anaingiaje huu ujinga wa kudandia watu wasiohusika sijui utaacha lini.
 
Tatizo lako we mburula hapa rais anaingiaje huu ujinga wa kudandia watu wasiohusika sijui utaacha lini.
Mburula ni wewe usiejua kuwa raisi ndio mwenye mamlaka ya ama kuongeza au kutokuongeza hiyo posho.

Acha kukurupuka!
 
Mburula ni wewe usiejua kuwa raisi ndio mwenye mamlaka ya ama kuongeza au kutokuongeza hiyo posho.

Acha kukurupuka!

Juzi huyu Simiyu kaleta thread hapa akijifanya yuko bungeni. Nikajiuliza kama Simiyu ni mbunge basi nchi yetu ina matatizo makubwa sana zaidi ya tunayoyafahamu. Kama tunaweza kuwa na mbunge mwenye mawazo kama ya Simiyu Yetu basi majanga hayataisha.
 
Kufuatilia mambo ya POSHO atakuwa amekosea sana. Kwani kwenye terms of reference alizotakiwa kuzisimamia katika upatikanaji wa KATIBA posho haikuwepo. Hapa inaonekana tutapata KATIBA ya kiposhoposho zaidi kuliko matakwa ya TAIFA.
 
Ccm na serikali yake ni chama cha matukio. Hivi tuwaulize walikwenda Dodoma kuunda kamati za jujadili posho au kujadili katiba?? Hii ni kuonyesha ni jinsi gani Ccn walivyo wawakilishi wa natumbo yao na familia zao. Watanzania tuamke tuseme Ccm sasa baaaasi.
 
Back
Top Bottom