Ningekuwa mimi ningeanza kumkata huyo mzungu. Yaani aina yake ya ufundishaji ni sawa na Omog tu. Muda wote anazuia. Kuanzia namba mbili mpaka namba nane anapanga mabeki na viungo wakabaji. Akicheza na Njombe Mji mfumo ni huo akicheza na Yanga mfumo ni huo. Yaani haujui hapa anapambana na ni timu kubwa au ndogo au hapa yupo ugenini au nyumbani.
Raha ya mpira jiachie sio kocha unakuwa mwoga mwoga wa kufungwa kila mechi unazuia hata muasisi wa huo mfumo Mourinho mwenyewe siku hizi kaacha kupaki basi. Watu wanaenda mpirani kuona soka la kitabuni na zaidi sana kushangilia magoli.
Timu kama simba ina kipa mzuri, mabeki wazuri, viungo wakabaji na viungo washambuliaji wazuri na mbele una Boko, Kichuya na Okwi halafu unakutana na timu kama Lipuli unaanza kudefendi unawaleta golini kwako kwani wasikudhuru?
Mbaya zaidi viungo washambuliaji unawaweka benchi unategemea nini. Mo bana kata huyo mtu timu mpe Djuma tushangilie magoli hata Pele alisema mpira ni magoli. Kocha nayeogopa kufungwa huyo sio kocha kabisa.
Acha timu icheze mpira ishambulie ikitokea kufungwa ni bahati mbaya kwani hata Barca, Real, Man U, Man Cityy n.k. mbona wanachezea tu vichapo mara kibao.