Panga malengo yako na yafanyie kazi

Joined
Jan 10, 2015
Posts
78
Reaction score
27
UMUHIMU WA KUPANGA MALENGO NA KUYAANDIKA

Habari ndugu mpenda mafanikio namatumaini yangu kuwa uko salama hadi wakati huu, niwakati mwingine tena tunakutana kwa mara nyingine kuhakikisha tunaufanya mwaka huu kuwa mwaka mwenye mafanikio kwetu, kipindi kilichopita tulijaribu kuangalia kuhusu malengo na jinsi ya kuanza kuandika malengo yako.

Leo tutajaribu kuangalia umuhimu wa kupanga malengo. Watu wengi sana bado wanateseka na haya maisha hawajui waaanzie wapi wala waishie wapi hayo yote ni kwa sababu hawana malengo, hii huwafanya kutojua wapi pakwenda.

Ngoja nikwambie kitu rafiki mafanikio yatakuwa ndoto kwako kama unaishi wakati huna malengo, yani mtu asiekuwa na malengo ni sawa na gari lilisilokuwa na matairi, halitakwenda popote, ni mwanzo wa mwaka sasa hebu angalia maisha yako ya miaka mitano iliyopita na leo yanafanana au yamebadilika?

Mazuri au mabaya kama hayajabalika rafiki utakuwa huna malengo au una shauku na kujisifia una malengo, wapo watu wengi sana ukimuuliza utaka nini kwenye maisha yako atakwambia nataka maisha mazuri, sasa ukimuuliza maisha mazuri yapi atakwambia yoyote tu!

Huu ni upofu, lazima uwe unataka kitu unachokijua. Hebu jiulize mtu akikuuliza sasa hivi ukipata bilion moja utafanya nini? Kwa kweli unaweza kuwa usijue utaifanyia nini kwa sababu malengo yako hujayaandika. Bado huna malengo bali una shauku. Leo nataka nikufundishe umuhimu wa kuweka malengo na kuyaandika.

1. UTAJUA WAPI UNAELEKEA

Faida ya kwanza ya kupanga malengo ni kujua wapi unaelekea, ukiangalia nasisitiza malengo yaliyoandikwa kama hujaandika maana kama hujui kwanini dayali imeandikwa mwaka 2015 ukadhan ni marembo rafiki imekula kwako, malengo yako lazima uyaandike, ukiandika utajua miaka mitano baadae utakuwa wapi kila siku ukiwa unasoma malengo yako unaona kule unakoelekea hata kama akija mtu akikwambia hujui basi wewe hutakata tamaa.

Nakumbuka kipindi naanza kabisa kujifunza biashara na kampuni ya Neptunus nilijiwekea malengo yangu juu ya biashara nilikuwa nakutana na vikwazo mara kwa mara lakini nilikuwa siachi, watu walifikiri nitaacha kwa sababu ndio nilikuwa naanza biashara lakini sikuacha hadi nilipofika ninapotaka hii yote ni kwasababu nilikuwa na malengo yaliyoandikwa.kama hujaandika malengo yako hutajua unaenda wapi.

Hebu jiulize maswali haya, miaka 5 ijayo utakuwa nani?, utakuwa na biashara gani? Utakuwa na familia ya watu wangapi? Utakuwa umeifanyia nn nchi yako? Jibu taratibu na uandike.

2.UTAJUA WAPI UMEISHIA

Hivi nikuulize hivi unajua uliyopanga mwaka jana mangapi yamekamilika n mangapi hayajakamilika? Siku moja kuna mtu mmoja alikuwa anahojiwa akaambiwa unaonaje mwaka 2014 akajibu nashukuru baadhi ya malengo yangu yametimia akaulizwa mangapi yametimia akabaki anatoa macho tu, huenda na wewe ukawa kwenye kundi hilo, hujui mangapi yamekamilika na mangapi hayajakamilika hiyo yote ni kwasababu huna amalengo na kama unayo basi hujaaandika, rafiki kama huna malengo mwaka ndio unaanza kaa chini anza kufikiria nini unataka kufanya mwaka huu 2015, na utafute dayali nzuri uanze kuandika, usiogope andika kila kitu ambacho unataka katika maisha yako kitokee, usiombe ushauri maana hayo ni mambo yatokayo moyoni mwako.

3.UTAJUA MUDA WA KUYAFIKIA

Rafiki katika maisha kila kitu kinawakati wake lakini kama utakuwa hunamalengo yaliyoandikwa lazima uishi kama kidudu, kidudu kinaenda tu ilimradi siku ziende, hebu jiulize miaka mingapi umesema maisha yako yatabadilika na hadi sasa yako pale pale, mara ngapi umesema utafikia malengo yako lakini uko hivyo hivyo, usimtafute mchawi, mchawi ni wewe mwenyewe, kamwe huwezi kuongeza juhudi katika kupambana katika maisha yako kama huna malengo yaliyoandikwa, malengo yaliyoandikwa yanakuwa kama uelekeo wa maisha yako, utatumia muda vizuri ili kuhakikisha unafikia malengo yako, lakini kama huna malengo yaliyoandikwa lazima muda unaisha na hujafanya kitu chochote, anza leo rafiki hujachelewa.

4.UTAJUA VITU UNAVYOVITAKA VITOKEE KWENYE MAISHA YAKO:

Ngoja nikuulize rafiki hivi unajua unataka maisha yako yaweje? Usiniambie unataka maisha mazuri hakuna maisha nazuri duniani, maisha mazuri yapi? Ukipanga malengo yako vizuri ukayaandika utajua kabisa vitu gani unataka katika maisha yako, yani mimi gari zote zipite ila ipo gari moja ikipita hiyo gari lazima mwili unisisimke, na ninajua hadi tarehe ya kuipata, kama huna malengo yaliyoandikwa katika maisha yako utakuwa kama chura, kila kitu unataka, yani hata leo mtu akija akikupa milion 20, unaweza badilisha mawazo ukazichezea zikianza kuisha ndio unaanza kukumbuka mawazo yako tayali umeshachelewa, lakini kama una malengo ambayo umeandika lazima hata ukipata pesa utajua wapi pa kuipeleka maana unajua vitu gani unataka.

5.UTAJUA UANZIE WAPI UISHIE WAPI

Wapo watu wengi sana wananipgia sim wananiambia Bassanga me ninalaki tano nifanye biashara gani? Huenda na wewe ukawa ni miongoni mwa watu hawa hujui wapi pakuanzia na nikweli hutajua wapi pakuanzia kwasababu hujui nini unataka kitokee katika maisha yako, kiugupi huna malengo tena yaliyoandikwa, lakin kama una malengo ambayo umeandika lazima utajua wapi unaanzia na wapi unaishia utaona maisha yako yanakuwa rahisi sana.

Ndugu msomaji ungana nami wakati mwingine tutaendelea kujifunza namna ya kupanga malengo.endelea kujifunza nami na kaa tayali kwa kupata semina zangu zitakazoanza hivi karibuni.

abtwahil@gmail.com
 
Kifikia mafanikio ni mchakato tata sana. Lakini inawezekana kama kuna dhamira ya kweli toka moyon.
 
Malengo yangu kwa mwaka 2014 ilikuwa ni kununua baiskeli ili inisaidie kwenda kibaruani..namshukuru Mungu kwani nimetimiza malengo yangu na sasa ninamiliki basikeli yangu mpyaaaaaa...dala dala tena bai baiii....
 
Malengo yangu kwa mwaka 2014 ilikuwa ni kununua baiskeli ili inisaidie kwenda kibaruani..namshukuru Mungu kwani nimetimiza malengo yangu na sasa ninamiliki basikeli yangu mpyaaaaaa...dala dala tena bai baiii....

Ubaiyaga daladala unakimbilia wapi? Wakati unapo pita ipo chini miguuni kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…