Sweya Makungu
JF-Expert Member
- Jun 11, 2023
- 508
- 601
PANGU PAKAVU TIA MCHUZI NILE
____________________________
✍🏽Yesu alianza kazi ambayo alikusudiwa na Mungu kuja kuifanya duniani alipotimiza miaka 30 . Na aliifanya kwa miaka 3 tu akaitimiza akafa akaondoka duniani.
Lakini, kabla Yesu hajaanza kazi hii aliyokusudiwa kuifanya, alikuwa Fundi Seremala tangu utoto wake.
Unaelewa hii maana yake ni nini?
Mungu hawezi kukupeleka katika hatua ya mafanikio au kazi aliyokusudia wewe uifanye duniani kabla haujapata ukomavu wa kulimudu jukumu hilo na wala hataki wewe ukae bila kazi ya kufanya wakati unasubiria kutimiza kazi ya ndoto yako...
Usilazimishe kuipata kazi au cheo unachotaka wakati hata hicho kidogo ulichopewa bado haujakimudu.
John Okelo (kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar), hakuwa Mwanasiasa mkubwa, isipokuwa alikuwa kuli (mlalahoi), mkulima, mkwezi na mbeba mizigo wa bandarini. Wakati Wanasiasa tunaowajua wakiwa bado wanasitasita, yeye na makuli wenzake ndio waliovamia Kituo cha Polisi na kuteka silaha na kuiteka Redio ya Taifa na kuanzisha Mapinduzi.
Umeelewa maana yake hii?
Haikuhitaji wewe uwe mtu wa kiwango au kada fulani ili uweze kutimiza mapenzi ya Mungu duniani. Dhamiri yako moyoni ndiyo kitu cha muhimu zaidi. Aidha, unaweza kuitendea dunia wema na bado dunia ikalazimisha kuufuta wema wako!
Hata tusipoiandika historia ya taifa hili vizuri bado watu wenye maarifa sahihi watawaeleza watoto wao ukweli halisi.
Paulo (Mtume mwenye elimu kubwa na mwandishi wa vitabu vingi kuliko wengine nyakati hizo), alikuwa ni muuaji, mtu mwenye dhambi, tena akilipwa na Serikali kwa kazi ya kuua, lakini ndiye leo hii amelishikilia Agano Jipya kwa Nyaraka zake nyingi alizoandika na maeneo mengi aliyozunguka kuueneza Ukristo.
Unapata picha gani?
Siyo lazima uzaliwe katika Familia Takatifu au uwe mtenda mema sana ndipo Mungu akuchague kwa kazi yake. Mungu akikutaka
atakuchukua hivyo hivyo ulivyo, haijalishi upo katika hali gani.
Mungu akikutaka uwaongoze watu siyo lazima uzaliwe au ukulie Ikulu ili uwe Kiongozi mzuri.
Majaliwa na wenzake wa Bukoba hawakuwa na elimu kubwa wala taaluma ya uokoaji, lakini walifanya maajabu ya kuokoa watu katika ajali ile ya ndege. Walifanya kazi hiyo kuliko hata wataalamu wetu, wabobezi wa ajali za majini. Umeelewa hapo?
Haihitaji elimu kubwa sana na kujua Lugha ya Kingereza ili uweze kutatua matatizo ya jamii yako. Kinachotakiwa ni ujuzi na maarifa ya kukabiliana na kuyamudu mazingira yanayokuzunguka. Elimu yetu iweke mkazo kwny maarifa na siyo lugha ya kikoloni.
Yesu aliuawa. Martin Luther King aliuawa. Patrice Lumumba aliuawa. Kwame Nkrumah aliuawa. Nelson Mandela alifungwa pia. Tundu Lisu alipigwa risasi. Magufuli aliwahi kulalamika kuwekewa sumu. Babu Seya na wanawe walifungwa maisha. Nikuambie kitu? Dunia haijali wala haiogopi kuwa wewe ni mwenye haki kiasi gani. Dunia inaogopa haki yako itawaharibia wao furaha yao ya uovu kiasi gani.
Nyakati za Mfalme Herode, aliyezuia mikusanyiko ni mtu mwingine na alisifiwa na aliyeruhusu mikusanyiko ni mtu mwingine na yeye alisifiwa pia.
Lakini, wasifiaji walibaki kuwa wale wale. Wale wale waliomshukuru Musa na kumtukana Farao wakati wanatoka Misri ndio hao hao waliomtukana Musa na kusifia vyakula vizuri vya Farao walipofika jangwani. Unajifunza kitu gani hapa?
Akili ya mwanadamu aliyepoteza matumaini na kubaki kumtegemea mwanadamu mwingine kwa ajili ya hatima ya maisha yake, huwa haijiendeshi yenyewe, bali inaendeshwa na mahitaji ya mwili na matukio.
Biblia inasema: "Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Mungu..."
"Kama haikuwa sawa kwangu, basi haiwezi kuwa sawa kwa mtu mwingine yeyote". Hakainde Hichilema.
_____________________________
© Mwl. Makungu, MS.
+255 743 781 910
JN. 10 Januari, 2023