Benokolongokonongose
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 213
- 52
Wadau, niko wilaya ya Masasi Mtandi niliyoyapata tangu jana na hata asubuhi hii nimeona vyema tugawane kwani kitamu kula na mwenzako.
Panya ni kitoweo kinachoheshimiwa sana na wamakuwa na wamakonde. Hapa nitazungumzia wamakuwa.
Mzee Anthon Marapi (92)anasema kuwa wamakuwa wanaishi muda mrefu kwa sababu ya afya njema inayopatikana kwa kumla panya.
Kwa mujibu wa maelezo yake anasema, panya ana virutubisho vingi kwa afya zetu.
Kwa mfano mafuta aliyonayo yanaboresha afya ya ngozi, moyo,kuondoa vidonda vya tumbo,kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kupambana na magonjwa ya zinaa, kuimarisha tendo la ndoa nk
Faraja Nankota ni msichana aliyepata talaka baada ya mumewe kumlazimisha aache kula panya akakataa. Faraja anasema ana ndugu zake wana umri mkubwa sababu ya kitoweo hiki. Ananipa mifano 2:
1. Babu yake ana miaka 102.
2. Shangazi yake miaka 87
Kwa hoja za kisayansi wanaomfahamu vizuri panya watujuze. Harufu yake imenishinda kumla nilivyotaka kujaribu. Ila wanabanikwa vizuri na kumwagiwa limao, chumvi, pilipili. Lol!