Panya anavyoboresha afya za Wamakuwa

Benokolongokonongose

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
213
Reaction score
52
Wadau, niko wilaya ya Masasi Mtandi niliyoyapata tangu jana na hata asubuhi hii nimeona vyema tugawane kwani kitamu kula na mwenzako.
Panya ni kitoweo kinachoheshimiwa sana na wamakuwa na wamakonde. Hapa nitazungumzia wamakuwa.

Mzee Anthon Marapi (92)anasema kuwa wamakuwa wanaishi muda mrefu kwa sababu ya afya njema inayopatikana kwa kumla panya.

Kwa mujibu wa maelezo yake anasema, panya ana virutubisho vingi kwa afya zetu.

Kwa mfano mafuta aliyonayo yanaboresha afya ya ngozi, moyo,kuondoa vidonda vya tumbo,kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kupambana na magonjwa ya zinaa, kuimarisha tendo la ndoa nk

Faraja Nankota ni msichana aliyepata talaka baada ya mumewe kumlazimisha aache kula panya akakataa. Faraja anasema ana ndugu zake wana umri mkubwa sababu ya kitoweo hiki. Ananipa mifano 2:

1. Babu yake ana miaka 102.
2. Shangazi yake miaka 87

Kwa hoja za kisayansi wanaomfahamu vizuri panya watujuze. Harufu yake imenishinda kumla nilivyotaka kujaribu. Ila wanabanikwa vizuri na kumwagiwa limao, chumvi, pilipili. Lol!
 
Kafanye ulioyaendea masas,na si kukashifu makabila ya watu,marupwenyuu
 
Kafanye ulioyaendea masas,na si kukashifu makabila ya watu,marupwenyuu
limbende, hiyo kashfa iko wapi? Mleta mada katoa maelezo tu juu ya ulaji wa panya na jinsi ulaji huo unavyoboresha afya za walaji, kisha akamalizia kuomba wataalamu wa lishe wachunguze kilichomo kwenye nyama ya panya, ili watu wengi zaidi wahimizwe kula nyama ya panya. Hakuna hata punje ya kashfa, in fact ni aina ya pongezi kwa wamakua na wamakonde kugundua lishe bora!
 
Last edited by a moderator:
Duu, kuna watu hawajui ugonjwa wa tauni?? Hata sayansi kimu hamkusoma, ohooo mitaala ilibadilishwa!!!!
 
Duu, kuna watu hawajui ugonjwa wa tauni?? Hata sayansi kimu hamkusoma, ohooo mitaala ilibadilishwa!!!!

mkuu tuelekeze ww basi tauni ni nini?
Pia sio kila kitu utajifunza shule, mimi sijasoma sayansi lakini sio kwamba sijui kila kitu kuhusu sayansi, nawe pia kuna vitu ukija kwangu , nitakushangaa kwa kutovijua mpaka leo!
Kumbuka elimu haina mwisho!
 
Kuna siku tunaenda Mtwara nilikaa na mzee mmoja anaitwa Mrope. Akaagiza watu wamletee pale masasi stendi panya. Wakamletea kupitia dirishani jamani walikuwa wengi. Akawaweka kwenye begi lake anatafuna mmoja mmoja na kunywe maji. Da nilitamani kutaka kuonja ila ile harufu mh. Akaniuliza kama huwa nakula panya nikamwambia hapana. Akasema "nyie vijana wa miaka hii mnashida sana kwa kuchagua vyakula". Ila kama mtu ameona ni kitoeo chukulia kobisi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…