Panya road, kwanini wapo Dar zaidi?

Enzi zetu sisi wa mwaka 47 kulikuwa na 'komando yoso'.
 
Enzi zetu sisi wa mwaka 47 kulikuwa na 'komando yoso'.

nakumbuka sana, walikuwa wakitamba maeneo yao pia kama magomeni, hizo criminal gangs zilikuja kumalizwa na Augustine Lyatonga Mrema (rip) alivyokuwa waziri wa mambo ya ndani na mpaka raisi Mwinyi akamteua kuwa naibu waziri mkuu ( nafikiri ndiyo aliyekuwa naibu waziri mkuu wa kwanza tangia kuanzishwa kwa republic yetu) kwa kazi aliyokuwa anapiga ...
 
Cheo cha naibu waziri mkuu kilibuniwa tu ili awe senior kwa mawaziri wezake kwani walikuwa wanamvimbia kwamba asiwaingilie kwenye wizara zao.
 
Kweli ufukara ni ujanja
 
Watu wanazaliana mtoto hajuwi cha mama wala baba
Uswahilini mitoto inazurula yenyewe mpaka saa nne usiku hakuna wa kumuliza
Mtoto mdogo miaka 12,13 anakesha kwenye singeli,kibao kata unategemea nini?

Ova
 
Udini umeingiaje hapa?. Huyo Samia alipata kura asilimia 98 kati ya asilimia 95 ya wapiga kura wote. Je alipigiwa na waislamu pekee. Punguza udini na ukabila.
 
Kwa sababu wanaume wa Dar wakitishwa na panya road wanatishika, huko vijijini ingepigwa yowe au pembe wanaume wangekusanyika kuwasaka hao road na ca moto wangekiona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…