Alisikika kamanda mkuu wa kanda ya kipolisi ya dar es salaam mwezi wa tano mwaka huu wa 2022 akisema wamefanikiwa kuwakamata vijana wasiopungua thelathini na moja 31 katika operesheni ya kuwasaka panya road iliyofanyika maeneo yote ya mkoa wa dar es salaam ambayo ilianza takribani tarehe 27/04/2022 huku wengi wakikamatwa maeneo ya chalinze, na kwa mujibu wa maelezo ya kamanda mkuu wa kanda ya Dar es salaam ACP Muliro alisema vijana hao walikamatwa wakiwa na vithibitisho kama redio, runinga, simu na baadhi ya vitu vingine ambavyo waliviiba kwa kupora kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam.
Pia walikamatwa na silaha kama mapanga , visu , marungu na silaha nyengine ambazo alizitaja wakati akizungumza na hadhira kwa siku iyo.
Pia ACP Muliro alitaja umri wa wahusika hao waliokamatwa ni kati ya vijana ambao wana umri kuanzia miaka 13 - 20 ambao walivamia na kupora mali za raia na kufanya mambo mengine ya uvunjifu wa amani katika maeneo tofauti tofauti ya jiji hili la Dar es salaam , ACP alimaliza kwa kusema taratibu za kisheria zitafuatwa ili wahusika wapewe wanachostahili.
Tukiangalia kwa undani zaidi tutagundua mambo kadhaa ambayo tutayoana juu ya uvunjifu huu wa amani uliofanywa na Panya road .
La mwanzo kabisa ni umri uliotajwa ni kati ya miaka 13 - 20 je ni kweli vijana hawa wenye umri uliotajwa vijana hawa hawana wazazi au walezi ? na kama wazazi au walezi wapo walichukua jitihada gani ya kimalezi juu ya watoto hawa wenye miaka 13 mpaka 20 , na kama watoto walikua wakaidi je walichukua hatua gani za kisheria kuwapeleka kwenye vyombo husika pindi walipowaona wanaenda kinyume na utaratibu uliowekwa .
La pili la kualiangalia ni kauli isemayo mtoto wa mwezio ni wako maana yake jamii kwa ujumla inawajibu juu ya kila mtoto kumjenga kimaadili hivyo basi tutajiuliza tena kutoka kwenye swali la kwanza kama wale vijana hawana wazazi au walezi kwa namna ilivyo vijana wale walizungukwa na jamii ambayo ni mimi na wewe je tulichukua jitihada gani za kutoa maadili kwa vijana wa aina ile tunaoishi nao kwenye mitaa yetu , na kama wamekua wakaidi mimi na wewe tumechukua hatua gani kupeleka taarifa sehemu zinapohusika ?
Kwa wazazi na walezi tuliowengi tunajitahidi kuwalea watoto wetu kwenye maadili yanayofaa ila kama tujuavyo kwa sasa walezi ni wengi kwa maana vijana au watoto huchukua tabia tofauti tofauti kutoka kwa marafiki mashuleni, kwenye michezo , kwenye mitandao (internet site ) na mitaani tunamoishi ni kweli wazazi au walezi tunajitahidi kuwapa watoto wetu maadili yanayofaa ila ukweli utabaki ya kwamba wazazi au walezi wengi hushindwa kuchukua hatua stahili pindi tuonapoona dalili ya kwamba watoto wetu wameshindikana tunawaonea huruma kwa kushindwa kuwafikisha kwenye vyombo vinavyohusika ila huruma hiyo ndiyo iliyotufikisha hapa iliyosababisha kuzaliwa kwa panya road tuliowashuhudia .
Kwa jamii ni mimi na wewe tumezoea kwenye mitaa yetu tunayoishi mtu anaweza akajua nyumba fulani au sehemu fulani wanauza madawa au bangi ila kwa kuwa ni jirani au ndugu au ana maslahi fulani na nyumba ile au sehemu ile hachukui hatua yeyote ya kudhibiti lile jambo la hovyo linalofanyika kwenye nyumba au sehemu ile, amini usiamini wale vijana tunaowacha mchana tukiwashuhudia wakivuta bangi hadharani au kwa kujificha kwenye maeneo ya jiji hili ndio sisi tuliosaidia kuzuka kwa panya road waliotikisa jiji hili.
Uhalisia ni kwamba wanaovuta bangi mchana kweupe maeneo ya mbagala na temeke dunia ikivaa koti lake usiku wataenda Ilala kuiba, kupora na uvunjifu wa amani na wale vijana wanaovuta bangi mchana manzese usiku ukiingia wataenda kijichi na kigamboni kuiba ,kupora na kwa wale vijana wanaovuta bangi mchana maeneo ya tandale, buguruni usiku utakapoingia watenda chalinze kuiba ,kupora na kufanya mengeni yasiyo ya kibinadamu , maana yake tunaowaona kwenye maeneo yetu wakivuta bangi mchana usiku ukifika hawawezi kufanya matukio kwenye maeneo yetu bali watafanya matukio kwenye maeneo ya watanzania wengine.
Kuna haja ya sisi kama wazazi na jamii kuchukua hatua mapema na si kulaumu jeshi la polisi, kwa jinsi tunavyoishi mitaani kwetu tunaacha kuziba ufa na tunawapa jeshi la polisi kazi ya ziada ya kujenga ukuta.
Kwa hali hiyo mimi na wewe tumeshindwa kuwafunza panya road na kwa bahati mbaya walimwengu nao wakasahau kuwafunza na ndipo wao panya wakatufundisha namna gani ya kuwafunza.
Ni kweli kwamba asiyesikia la mkuu huvunjika guu lakini tusipokua makini tutamaliza miguu mingi ya watoto wetu ambao huenda tukijitahidi kuwanusuru kwenye mitaa yetu tunayoishi huenda wao ndo wanastahili kuwa wakuu wa baadae.
Kwa maana hiyo tukiacha tena kuwafunza vijana wetu yatajirudia tena kwenye maeneo yetu yalianza ma mbwa mwitu ya mbagala na temeke miaka ya 2005 mpaka 2008 yakaja mapanya road ya chalinze mwaka huu 2022 na huenda safari hii tukashuhudia masimba majoka na machui ya masaki kama tusipobadilika.

Upvote
0